MANJI KUMBURUZA MAKONDA MAHAKAMANI.

Baadhi ya Nukuu kutoka katika mkutano wake na wanahabari baada tu ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda Kumtaja katika Orodha ya wanaohitajika Kufika Kituo cha pilisi kwa Tuhuma za Madawa ya kulevya.

"Kifungu cha 66 na 32 vya katika Katiba ya nchi vinaeleza haki
 zangu na vinazilinda. Nataka nimshtaki Makonda Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunihusisha na madawa. Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. (Makonda huniamkia kaka) Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.......


Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika (asif wameconfirm mimi nauza madawa), nitawashtaki pamoja na Makonda. Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali......

Hawezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki. Zipo njia za kushughulikia vitu. (Makonda amesema kuwa ametuita tumsaidie kufichua wauza unga). Mbona hajamuita Kadinali Pengo? Kama unataka msaada omba msaada sio unaagiza msaada......

Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamshtaki mahakamani nikamdai shillingi moja, nikamshinda. Unanihusisha mimi kwa jina langu niloachiwa na baba kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako? Sasa ajiandae kupanda mahakamani. Nitamshtaki.!"
Nini maoni yako??

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.