Friday, February 10, 2017

MBOWE APUUZA WITTO WA RC MAKONDA,ATANGAZA KUTOKWENDA


"Mbowe amengumza na waandishi wa habari, asema Makonda hana mamlaka ya kumuita"

Shikamoo Kamanda!


Mbunge wa Jimbo la Hai Freeman Mbowe amezungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma hivi sasa.

Freeman Mbowe amesema hatafika polisi kwa kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Amekanusha vikali tuhuma za kuhusika na biashara au kutumia madawa ya kulevya.
Anasema wao kama chama wanaunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Anasema kuwa serikali imechelewa kuendesha vita hiyo.
Asema CHADEMA na kambi ya upinzani kwa ujumla haiungi mkono mapambano hayo yanayoendeshwa kwa hila.
Makonda hana mamlaka ya kumpa wito mtu kwenda polisi kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa,”amesema Mbowe.
“Makonda amemchafulia jina langu, chama, familia na upinzani.”
Anasema RC anachofanya ni kuwaepusha watuhumiwa wa dawa za kulevya na mkono wa sheria.
Anasema atamfungulia mashitaka ya kumchafulia jina lake kwa kumhusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Anasema yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote endapo njia sahihi zitatumika.

No comments: