Monday, February 6, 2017

POLISI WAADHIMISHA SIKU YA KUPINGA UKEKETAJI KWA KUPOKEA VIFAA VYA KISASA VYA KUKUSANYA TAKWIMU ZA UKATILI KUTOKA CDF

Kamishna wa Polisi Jamii Tanzania CP Mussa .A. Mussa akipokea baadhi ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya kukusanya na kuhifadhi Taarifa za Ukatili wa aina mbalimbali vifaa ambavyo vimetolewa na shirika la utu wa Mtoto CDF kwa msaada wa UNFPA makabidhiano ambayo yamefanyika makao makuu ya polisi wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga Ukeketetaji nchini.

Akizungumza wakati wa Hafla Hiyo Fupi Kamishna CP Mussa A Mussa amesema kuwa Jeshi la pilisi nchini kupitia Dawati la jinsia sasa wamejipanga kupambana na aina yoyote ya ukatili kwa watoto na watanzania wote hivyo sasa ni wakati wa mashirika mbalimbali na wadau kujitokeza kwa wingi katika kutoa msaada wa Vifaa vya kisasa kama Vilivyotolewa na CDF ili kufanikisha adhma ya serikali hii ya kupambana na ukatili wa aina zote.

Akizungumzia siku ya kupinga Ukatili wa ukeketaji nchini Kamishna Huyo amesema kuwa sasa ni wakati wa watanzania kuachana na mila potofu na kupinga kwa nia moja watu wanaoendeleza Mila za ukeketaji kwani ni kinyume kabisa na Haki za binadamu nchini ambapo amesema kuwa Jeshi la polisi pamoja na changamoto zilizopo bado wanapambana kwa nguvu katika Mikoa ambayo imekuwa sugu katika hilo ili kuhakikisha kuwa wanatokomeza hali hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Bernad Luoga akizungumza wakati wa Hafla hiyo ya maadhimisho ya siku ya kupinga Ukeketaji nchini shughuli iliyokwenda sambamba na makabidhiano ya vifaa maalumvya ukusanyaji wa Takwimu za ukatili kwa jeshi la polisi Vifaa ambavyo vimetolewa na Jukwaa la Mtoto Tanzania CDF kwa msaada wa  UNFPA.

Akizungumza wakati wa makabishiano hayo Mkuu huyo wa wilaya ya tarime ambapo ndipo mradi wa vifaa hivyo unaanzia kufanya kazi amesema kuwa Wilaya ya tarime pamoja na kuonekana kuwa ukeketaji umepungua kulingana na Takwimu za Hivi karibuni lakini bado Changamoto hiyo ipo kwa kasi katika maeneo kadhaa Huku akizitaja baadhi ya sababu kubwa zinazofanya vitendo hivyo kuendelea.

Baadhi ya sababu hiyo ni pamoja na Umaskini ambao umepelekea Tendo la ukeketaji kuwa kama chanzo cha mapato kwa wale ambao wanatekeleza tendo hilo yani mangariba,ambapo amesema kuwa baadhi ya maeneo wamekuwa wakikeketa hadi kufikia elfu ishirini kwa mtu mmoja ambayo ni pesa nyingi kwa Mtu wa kijijini na endapo atapata watu wengi wa kukeketa wanaitumia kama njia yao ya kujiingizia kipato.

Ameongeza kuwa pia ipo changamoto ambayo viongozi wa maeneo hayo wanaotaka kuingilia kati mila hiyo wanayokutana nayo ikiwa ni pamoja na Kutishiwa kuuawa na wengine kupigwa na wanavijiji ambao wanaamini katika tendo hilo jambo ambalo amesema kuwa limekuwa likiwapa changamoto kubwa askari lakini pia viongozi wanaotaka kuondoa hiyo mila katika maeneo hayo.

Aidha amesema kuwa Vitendo vya ukatili katika wilaya ya Tarime vimepungua kwa kiasi japo kuwa eneo hilo limeendelea kuonekanan kama eneo hatarishi kwa kuwa wafanyaji ukatili wa maeneo hayo wamekuwa wakifanya kweli na kwa kasi kubwa kulinganisha na Mikoa mingime.

Pamoja na Hayo Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru shirika la CDF kwa kuwekeza katika maeneo hayo kutaka kupambana na ukatili kwani ni jambo la kuigwa kwa mashirika mengine yenye nia ya kufuta ukatili nchini kuwekeza katika meneo ambayo yana ukatili uliokithiri
Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia nchini Tanzania Afande DCP Maria Nzuki akitoa shukrani zake kwa Mashirika ya CDF na UNFPA waliofanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo.


Kamishna wa Polisi Jamii Tanzania CP Mussa .A.Mussa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo akizungumza

Mwakilishi kutoka UNFPA ambao ndio wanunuzu wa Vifaa hivyo Bi Christine Kwayu akizungumza wakati wa hafla hiyo
Picha ya Pamoja baada ya shughuli hiyo.



No comments: