Friday, March 31, 2017

DR SLAA AANZA KUICHOKONOA SIASA YA TANZANIA,AZUNGUMZIA UONGOZI WA RAIS MAGUFULI


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dkt Willbrod Slaa alipozungumzia utendaji kazi wa Rais Magufuli amesema kuwa watu waelewe hakuna nchi hata moja ambayo kiongozi atakubalika na watu wote kwa asilimia 100.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania akiwa nchini Canada Alhamisi hii, Dk. Slaa ambaye amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.

Dkt Slaa alisema wako watu ambao maslahi yao yataguswa kwa namna moja au nyingine hivyo lazima watapiga kelele.

“Hatua zote zimechukuliwa,zinapaswa kuwa endelevu. Kwa bahati mbaya mchwa wengine waliopenya mpaka ndani ya Ikulu na Serikali na huwezi kufagia Serikali nzima kwa siku mmoja. Kwa jinsi Rais ambavyo hayumbi na wala hayumbishwi, nina hakika atafikia malengo na kurudisha Taifa kwenye misingi ya tunu za Taifa ya uwazi, ukweli, uadilifu, kuheshimiana na kuthaminiana na hasa kujali utu,” alisema.

“Hii ndiyo hali ambayo Rais Magufuli kila siku anaiita ‘Transition’ (kipindi cha mpito). Tutafika tu, tunatakiwa kuwa wavumilivu na wenye uzalendo wa kweli ana nia njema ya kufikisha Taifa mahali pazuri. Hii inahitaji kuweka pembeni maslahi yetu binafsi kama mtu mmoja mmoja, viongozi wa Serikali au hata wa kisiasa.”

No comments: