Saturday, March 25, 2017

Hospitali ya Kimataifa ya Aga khan imeanzisha mfumo maalum wa utoaji wa tiba kwa akina mama



Pichani ni  Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Aga Khan Olayce Lotha
NA KAROLI VINSENT
HOSPITAL ya Kimataifa ya  Aga khan kwa kushirikiana na Daktar bingwa wa masuala ya akina mama  kutoka Uengereza imeanzisha mfumo maalum wa utoaji wa tiba kwa akina mama wenye  uvimbe katika milango ya kizazi bila kuwafanyia upasuaji mkubwa ambapo zoezi hilo litakua endelevu lengo ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikai wananchi wengi  .


Akizungumza na waandishi wa habar Dkt,bingwa wa masuala ya akina mama ambaye pia mtaalamu wa masuala ya mionzi kutoka Uengereza,Nigel Hancking alisema kuwa huduma hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo imebainika kuwa tatizo hilo huwaathiri zaidi akina mama kuanzia umri wa miaka 20 hadi 50.


Amesema kuwa,ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo ni vyema kutokoa madakrati nchini Tanzania kwenda kusoma Uengereza ili kuweza kutoa huduma nzuri kwa wananchi  pamoja na kupunguza gharama za matibabu kwa ajili ya kuwasafirisha  madaktar kutoka Uengereza.


Dkt,Nigel amebanisha kuwa kutokana na changamoto hiyo wameamua kutoa huduma ambayo inaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa sana kuondoa tatizo hilo kwani  wanatoa huduma hiyo bila kuwafanyia wagonjwa upasuaji mkubwa.


“Tunatoa huduma hii kwa ajili ya akina mama ambao wamepatwa na tatizo hili tena bila kuwafanyia upasuaji mkubwa ambao hulazimika kukaa siku mbili hospitalini hapa na kurudi nyumbani tena wakiwa wamepona kabisa na wengine hupata maumivu madogo mdogo.


Kwa upande wake Daktar Bingwa Magonjwa ya kina mama na uzazi kutoka Hospital ya Aga Khan  Lynn Mosh amesema huduma hiyo ya matibabu kwa wagonjwa yana usalama mzuri kwa mgonjwa kwani huweza kuwekewa chembechembe kwenye mishipa ya damu  ambazo zinaweza kufanya uvimbe huo ukasinyaa  bila ya kufanyiwa upasuaji.


Aidha alisema kuwa matibabu hayo yana gharimu sh.mill.7 kubwa ambapo wamejitahidi kuzipunguza lengo ikiwa ni kuweza kuwafikia wananchi wengi  ambao hawana uwezo  wa kuweza kutimiza kiwango hicho,ambapo hadi sasa wameshawafanyia watu 9.


“Ni zoezi la muda mfupi kati ya dakika 10 hadi 15 ambapo mgonjwea hulazimika kukaa hospitali kwa siku mbili ambapo akiruhusiwa kuondoka nyumbani anaweza kuendelea na kazi zake kama kawaida na wengine hupata maumivu  kwa muda wa wiki moja”alisema Dkt,Lynn.


Naye Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Aga Khan Olayce Lotha alisema kutokana na kua zoezi hilo linafanyika kwa mara ya kwanza katika hospital hiyo,wameamua kutoa tarifa kwa vituo vyao mbali mbali vilivyopo nchini ili kuanza uchunguzi na kutoa na kupata kesi ambazo zinaweza kupatiwa matibabu.


Aidha alisema,kutokana na zoezi hilo kua na matibabu ya gharama za juu wameamua  kushirikiana na taasisi za bima za bima ya afya ili kuhakikisha kama wanaweza kuchukua gharama za matibabu ili aweze kuwasaidia wagonjwa ambao wanahitaji tiba hiyo.


No comments: