Thursday, March 2, 2017

JUKATA WACHOKOZA TENA KATIBA MPYA,SASA WAMBEBESHA ZIGO LA LAWAMA RAIS MAGUFULI


Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukwaa La katiba Tanzania
                                         Na Vicent Macha 
Jukwaa la katiba nchini Tanzania leo limezindua mkutano wake utakaodumu kwa siku mbili ukiwa na lengo la kuitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoa mustakabadhi wa katiba mpya baada ya  kudai kuwa mchakato ulianzishwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mh. Jakaya Mrisho Kikwete na kuhitaji serikali ya awamu ya tano kuweza kumalizia mchakato huo.


JUKATA wameeleza kuwa Mh John Pombe Joseph Magufuri wakati akizindua bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania alisema kuwa ninajua tunakiporo cha katiba mpya  hivyo walitakiwa wabunge kuweza kumkumbusha mheshimiwa Raisi juu ya kauli yake ya kuwa kuna kiporo cha katiba mpya huku wakishtushwa baada ya kuona hakuna hata mbunge mmoja aligusia swala la katiba mpya.

Mkutano huo uliyoudhuriwa na watu mbalimbali kutoka vyama mbalimbali ya siasa nchini na asasi zisizo za kiselikali na Maprofesa pamoja na waandishi wa habari lengo ni kuweza kupaza sauti kwa pamoja ili kuweza kuhamasisha wahusika wa tatizo hilo.

Akiongea kwa msisitizo Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bwana Deusi Kibamba alisema wananchi wote kwa sasa wapo makini na kusubiri mchakato huo huku akisema kuwa  wakati ni sasa kwa maana hakutokuwa na muda tena wa kuweza kujadili mambo ya katiba kwa maana ikifika 2019 serikali itakuwa bize na chaguzi za selikali za mitaa na ifikapo 2020 taifa zima litakuwa bize na uchaguzi mkuu na halitakuwa na muda wa kujadili katiba.

Pia aliongezea kwa kusema vyama vya siasa vinatakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye hili kwa maana ipo kwenye ilani ya vyama vyao iliwemo chama tawala cha CCM kilisema kuwa kikishinda kitahakikisha kinaipatia taifa katiba mpya vivyo hivyo na chama kinachounda umoja wa UKAWA pamoja na ACT wazalendo.Ila kwa kuwa CCM ndio kimeshinda basi kinatakiwa kutimza azma yake ya kuwapatia wananchi katiba mpya kwa kuwa ni haki yao ya msingi.
Aidha Jukata wanasikitishwa na kwa kauli ya Rais aliyosema kuwa wakati anaomba kura hakusema kuwa atabadilisha katiba iliyopo kwa kauli hiyo jukata wameomba  kujua kwamba wakati anazindua bunge aliposema kuwa najua kuna kiporo cha katiba alikuwa akiongelea kisiasa tu au alikuwa akimaanisha kweli.


Katika Hatua nyingine Jukata wamepongeza  jitihada za mzee Warioba kwa kuwasilisha katiba yenye maoni ya wananchi na sio katiba iliyopendekezwa kwa kuwa katiba iliyopendekezwa ilikuwa na mapungufu mengi na kingine katiba hiyo ilikuwa ikiwapa nguvu kubwa chama tawala.

No comments: