Saturday, March 18, 2017

JUKATA WAMKOMALIA RAIS MAGUFULI,WATAKA MCHAKATO WA KATIBA UREJESHWE HARAKA

 Jukwaa la Katiba Tanzania leo limemtaka Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa nafasi yake kulitangazia Taifa rasmi Tarehe rasmi ya kurejeshwa kwa mchakato wa kupata katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuchapishwa kwa tangazo lake katika gazeti maalum la serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa JUKATA Bwana Deus Kibamba wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maamuzi ya mkutano mkuu  uliomalizika hivi karibuni uliokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja na wadau mbalimbali jinsi ya kurejesha mchakato wa katiba Tanzania ambao unaoinekana kukwama,
Kibamba amesema pamoja na maazimio mbalimbali yaliyamuliwa na wadau wa mkutano huo umeona kuwa Rais wa Tanzania kwa nafasi yake ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kurejesha mchakato wa katiba nchini ili watanzania waendelee na mchakato huo baaada ya kusimamishwa kupisha uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka Juzi nchini.


Kibamba amesema kuwa Rais pamoja na waziri husika wanawajibu wa kufufua mchakato wa katiba kwa sasa kwani umetumia fedha nyingi za watanzania na mchakato huo haujakamilika.

Aidha kibamba amesema kuwa mkutano huo kwa kauli moja uliamua kuchagua wajumbe mbalimbali wanaohusika na maswala ya katiba kufanya mchakato wa kukutana na Rais wa Tanzania kuhakikisha kuwa wanamshawishi na kumpa maoni yao kuhusu jinsi ya kufufua mchakato huo kwani ni ukweli kuwa watanzania sasa wanahitaji katiba mpya ambapo pia Jukata wametangaa kusaidiana na serikali katika mchakato huo wa katiba ikiwa ni pamoja na kuhamasisha watanzania kuwa na hari tena ya kujitafutia katiba mpya.





No comments: