Friday, March 24, 2017

KAMPUNI YA SIMU YA ITEL YATOA MISAADA KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA MUGABE SINZA DAR ES SALAAM

Kampuni inayotengeneza simu za mkononi za Itel lmetoa misaada kwa wanafunzi wenye mahitaji katika shule ya sekondari ya Mugabe iliyopo Sinza  jijini Dar es salaam. Misaada hiyo ikiwemo madaftari kalamu za wino na mabegi zaidi ya 100, misaada hiyo  na imepokelewa na makamu mkuu wa shule hiyo Bw. Elias Kambawala na kugawiwa kwa wanafunzi hao. Baada ya zoezi la ugawaji wa zawadi hizo pia kulikuwa na michezo tofauti tofauti kama mashindano ya mpira wa miguu, kushindana kuimba pamoja na kucheza miziki mbalimbali.

Afsa masoko wa Itel akiongea na vyombo vya habari jinsi walivyotoa misaada kwa wanafunzi shule ya mugabe
Saifoni Asajile ni meneja masoko wa kampuni ya Itel Tanzania amesema  kuwa zoezi hilo limekwenda vizuri kama lilivyopangwa na wanfunzi wamepokea kwa furaha kubwa sana huku pia alisisitiza zoezi hilo sio kama ndio limeanza kwa shule hiyo tu. Bali ni zoezi linafanyika kila mwezi katika shule mbalimbali lengo likiwa ni kuwapa fursa hata kwa wasio na uwezo kuona wanathaminiwa katika jamii.Kama mwezi uliopita waliweza kuwa shule ya msingi  air wing kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum na zoezi bado linaendelea kwa mikoa yote nchi nzima.

Makamu mkuu wa shule bw. Elias Kambawala akielezea jinsi alivyoweza kupokea misaada hiyo
Makamu mkuu wa shule hiyo Bw Elias Kambawala amesema kuwa wamepokea misaada hiyo na imeweza kuwafikia walengwa ambao ni wanafunzi wenye uhitaji. Pia aliongezea kusema wanafunzi hao walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa vifaa vya taaluma hiyo na kwa sasa wameweza kuipata misaada hiyo itawapa motisha ya kupenda kusoma. 
Meneja masoko akigawa zawadi kwa wanafunzi mbalimbali
Baadhi ya wanafunzi wakiongea na Habari 24 wameishukuru Kampuni ya ITEL kwa msaada huo huku wakiomba kwa Taasisi nyingine kuiga mfano huo wa Kuwasaodia ili waweze kusoma kwa Bidii zaidi.
Makamu mkuu wa shule na wanfunzi wakiwa wameshika zawadi walizopewa 


Mwanafunzi Octa akionyesha umahili wake katika kuimba wimbo wa Nandy  one day

No comments: