Monday, March 20, 2017

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji, Prof Zakalia Mganilwa amewataka umoja wa wanake katika chuo hicho UWANIT kuwa wabunifu

Mkuu wa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) PROF Zacharia Mganilwa  akizungumza na wanachama wa umoja wa wanawake NIT (UWANIT) katika sherehe za uzinduzi wa umoja huo. Prof. Mganilwa ameutaka umoja huo kuwa wabunifu kutafuta vyanzo vya pesa na pia kuwa wamoja kwani bila kufanya hivyo umoja huo unaweza kufa.



NA MWANDISHI WETU;

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji, Prof Zakalia Mganilwa amewataka umoja wa wanake katika chuo hicho UWANIT kuwa wabunifu ili waweze kuendesha umoja wao bila kutegemea wahisani, akisisitiza kuwa kama wasipokuwa wamoja na wabunifu chombo hicho kinaweza kukosa pesa na mwisho wake unaweza kuwa mbaya.


Wito huo ameutoa katikati ya wiki wakati akizindua kwa mara ya kwanza umoja wa wanawake wa chuo hicho (UWANIT) katika Hotel ya GM elegance iliyopo Sinza Jijini Daresalaam.


Prof Mganilwa amesema ameshuhudia umoja wa namna hiyo unavyokufa kwa kukosa pesa,lakini hataki kuona hilo likitokea kwa umoja wa UWANIT kwani anaamini wanaweza kubuni miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato na kwa kuwa kinamama ndio watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii wataitumia mitandao hiyo kutangaza shughuli zao za kibunifu jambo likalowafanya kufika mbali.


“Duniani kote Mwanamke ni nguzo muhimu katika malezi ya familia nami naamini kupitia umoja huu mtakua walezi wazuri wa Chuo chetu hasa ukizingatia hii ni Taasisi ya Elimu ambayo inalea wanafunzi walio katika kipndi cha kushawishika kirahisi,hivyo kupitia umoja huu wekeni utaratibu utakaoweza kusaidia wanachama kujikwamua kiuchumi,kitaaluma lakini pia mkumbuke namna ambavyo mnaweza kuwainua hata wanafunzi wetu wale wenye skills mbalimbali ili kuwaandaa kuwa walezi bora.” Alisema Prof Mganilwa

…AKUBALI OMBI LA KUWA MLEZI WA UMOJA WA UWANIT

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Chuo amekubali kwa mikono miwili ombi la kuwa Mlezi wa Umoja huo, na kwamba yuko tayari kutoa msaada wowote ikiwemo ushauri na hata mengineyo kwani anaamini umoja huo ni mzuri kwa mustakabali wa maendeleo ya chuo.

“Nimesoma malengo yenu, kwa kweli ni mazuri na yamelenga kukisaidia Chuo kusonga mbele, nimefurahishwa sana na jambo hili niwaahidi Full support yangu; naamini mkifanikiwa nyie itakuwa faraja kwa Jumuiya nzima ya NIT” aliongeza

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake NIT (UWANIT) Bi Joyce Bakari Mpunga akizungumza na wadau walioshiriki katika uzinduzi huo. katika umoja huo una jumla ya wanachama 96,
 Awali akisoma hutuba ya ufunguzi kwa mgeni rasmi, Mwenyekiti wa sasa wa umoja huo ambaye pia ni Mkuu wa idara ya Rasilimali watu na utawala Bi. Joyce Bakari Mpunga amesema wazo la kuunda umoja huo lilikuwa ni kuwawezesha wanawake wa Jumuiya ya NIT kujitengenezea kipato cha ziada nje ya mishahara kwa kupatiwa mafunzo yatakayowasaidia kujishughulisha na ujasiliamali.

Ametaja malengo mengine kuwa ni kuboresha mahusiano mazuri mahala pa kazi; kusaidiana katika masuala ya kijamii katika shida na raha pamoja na kuelimisha na kuhamasisha mazingira bora ya ufanyaji kazi kwa nidhamu na uwajibikaji kazini.

Aidha akizungumzia idadi ya wanachama wa umoja huo, Bi Mpunga amesema kwa sasa Umoja huo unawanachama 96 ambao kama umoja huo utasimama basi itasaidia sana kuboresha hali za akina mama chuoni hapo na hivyo kufanya Chuo kupata mafanikio mengi kwani bila shaka watafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.


Hiyo ni Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chuo cha Taifa cha usafirishaji, Wanawake kuanzisha Jumuiya yenye madhumuni ya kusaidina katika raha na shida. Fullhabari ilikuwepo katika eneo la tukio na kujionea mafunzo mbalimbali yakitolewa yakiwemo ya ujasiliamali pamoja na ya kubadili fikra/matzo yaliyotolewa na YEMCO.

No comments: