Thursday, March 9, 2017

MKUU WA WILAYA YA KISARAWE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MKOA WA PWANI


 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda (katikati), akihutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani  Kisarawe jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile, akipima shinikizo la damu katika maadhimisho hayo.
 Diwani wa Kata ya Kisarawe, Abel Mudo akipima afya.

 Ofisa Mikopo wa Benki ya Equity, Nelifyage Mbwilo (kulia), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (wa pili kushoto), wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya wajasiriamali katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile.
 Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Wilaya ya Kisarawe wakionesha kazi wazifanyazo.
 Wajasiriamali wakiwa na bidhaa zao mbalimbali wanazozalisha.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness (katikati), akiserebuka na wanawake katika maadhimisho hayo.
 DC Seneda akiserebuka na wanawake. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Winamwanga Caltural Heritage Association, Mwajuma Motto.
 Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mussa Gama (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya hiyo, Happyness Seneda.


 Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wadau wa maendeleo kutoka Taasisi ya Jumuiya ya Miradi ya Maendeleo Kisarawe na Ilala(JUMIMAKI) wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Katikati ni Katibu wa Hatibu Baruti.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneka (katikati kulia na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Skauti wakati wa maadhimisho hayo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Ntela Mwampamba (kushoto), akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Madiwani wa Wilaya hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Maadhimisho yakiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Winamwanga Caltural Heritage Association, Mwajuma Motto akisoma risala kwa niaba ya wadau wa maendeleo wa wilaya hiyo.
Mdau wa maendeleo, Christina Lusian akisoma risala 
mbele ya mgeni rasmi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Yusta Milinga akizungumzia ukatili wa kijinsia kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Seneda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 61,550 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani humo iliyotolewa na Benki ya NMB.
Wadau wa maendelea wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo baada ya kukabidhi msaada wa magodoro na vifaa vingine vyenye thamani ya sh.700,000.
Mkurugenzi wa Taasisi ya  Tanzania Kwanza Foundation, Hidaya Chomvi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya baada ya kumkabidhi zawadi.
Brass Bandi ya Magereza ikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameziagiza Halmshauri zote za mkoa huo kuhakikisha kuwa zinatenga asilimia tano ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake.

Agizo hilo lilitolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani  humo jana. Ndikilo alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.

"Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo hazitatekeleza wajibu wahakikishe wanajitahidi kufanya jukumu hilo muhimu kwa maendeleo ya wanawake wa mkoa huo" alisema Seneda.

Alisema katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, Serikali imeanzisha Benki ya Wanawake Tanzania, mifuko mbalimbali ukiwemo  mfuko wa maendeleo ya wanawake (WDF) pamoja na kuhamasisha uanzishaji wa Saccos, vikundi vya uzalishaji mali na Vicoba na kwa kupitia fursa zilizopo kuwawezesha wanawake wajasiriamali kupata mikopo yenye masharti nafuu.

Alisema katika mkoa huo kuna jumla ya vikundi vya uzalishaji mali 1, 350 vyenye wanachama 5,411 lengo likiwa ni kumuwezesha mwanamke kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.

Seneda akizungumzia wilaya yake alihimiza suala zima la elimu na kuwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kusimamia watoto wao na kupiga vita mimba za utotoni na kuwaoza watoto wao.

Alisema serikali haitamvumilia mzazi au mlezi yeyote atakayebainika kuozesha mtoto wake na mtu atakaye mpa mimba mwanafunzi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: