Thursday, March 30, 2017

Mtangazaji Clouds Afukuzwa Kazi kwa Kumtaja Makonda Kwenye kipindi,TEF wapongeza Hatua Hiyo

Taarifa Kuhusu Kutoandika Habari za RC Makonda

Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia.

Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.

Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu.

Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.

Bodi inakipongeza Kituo cha Clouds kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda.

Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.

Theophil Makunga,
Mwenyekiti TEF

Imetolewa Leo,
Machi 30, 2017

No comments: