Tuesday, March 7, 2017

Tigo yashirikiana na Milvik kutoa huduma za bima ya afya wanazomudu wateja


Meneja mkazi wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin(kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi kwa kutumia Tigopesa ijulikanayo kama Bima Mkononi, Pembeni yake ni Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel.

Mteja aliyenufaika Melikizedeki Nyalufujo mkazi wa kimara , akitoa ushuhuda

Mteja aliyenufaika na huduma ya Bima Mkononi kwa kutumia Tigo pesa , Hawa Ramadhani mkazi wa Kibaha Maili Moja akiongea na waandishi wa jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi. Wengine kutoka kushoto Meneja mkazi wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin, Mteja aliyenufaika Melikizedeki Nyalufujo mkazi wa kimara na Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel.

Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel(kulia) , akiongea na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi kwa kutumia Tigopesa ijulikanayo kama Bima Mkononi, Pembeni yake ni Meneja Mkazi wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin.

 Dar es Salaam, Machi 2017- Moja ya makampuni yanayoongoza kwa bima ndogo Tanzania  ambayo inatumia teknolojia ya simu za mkononi katika kutoa huduma za bima ya afya inaleta mapinduzi katika sekta ya ndani ya  bima  kupitia TigoPesa.  
Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na kampuni Milvik ziliingia katika makubaliano ya kutoa Huduma hii tangu mwaka jana kwa kutoa Huduma ya bima kwa simu za mkononi ijulikanayo kama Bima Mkononi ambayo inatoa bidhaa za kipekee na za hali ya juu kama vile,bima ya maisha, ugonjwa na ajali kwa wateja wanaotumia Huduma ya TigoPesa.
Ikiwa na wateja hai zaidi ya 200,000, BimaMkononi ni mfumo mpya wa bima kwa Watanzania wa kawaida ambayo inawawezesha kuwakinga dhidi ya matukio yasiyotarajiwa yanayoweza kuwa na athari kubwa kwa hali ya kifedha kama wasingekuwa wamejiunga na huduma au mpango huu wa bima.  
Tayari BimaMkononi ishalipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 27 katika miezi sita iliyopita.
Hawa Ramadhani  ambaye ni mama wa watoto watatu  kutoka wilaya ya Kibaha, mkoa wa Pwani  ni mmoja wa wanufaika wa BimaMkononi. Akieleza jinsi BimaMkononi  ilivyobadilisha maisha yake alisema; “Nilikuwa nimelazwa katika Hospitali ya tumbi kwa siku 21 na baada ya kuruhusiwa kutoka, niliwasilisha  taarifa za hospitali katika duka la Tigo la huduma kwa wateja na nilifurahi waliponiita baada ya siku tatu  na kupokea  kitita cha 840,000/-! Alisema kuwa aliambiwa  bima  imemfidia kwa kipindi  alichokuwa amelazwa hospitalini.
“Kwa pesa hizo niliweza  kulipia ada ya shule ya watoto iliyokuwa imebaki, pamoja na kukuza  biashara yangu ndogo,” alisema na kuwashauri wale ambao hawajajiunga na mpango huu  kufanya hivyo ili wavune faida.
Mwingine ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia cha St. John,  Dar es Salaam Melikizedeki Nyalufujo ambaye ni mnufaika mwenye furaha wa BimaMkononi baada ya kupokea 86,000/- kufuatia kulazwa kwake hospitalini kwa siku mbili kutokana na jeraha alilolipata.
“Mara ya kwanza nilipoelezwa kuhusu BimaMkononi nilikuwa na wasiwasi lakini nilijiunga. Hata hivyo nilishawishika kujiunga baada ya kupokea fedha hizo ndipo  nilithibitisha kwamba ilikuwa ni kweli. Ankara za hospitali  ilikuwa ni 16,000/-; hivyo kwa fedha  hii ya ziada  niliweza kulipia  gharama nyingine  kama vile kujikimu  chuoni, kununia vifaa  vya masomo na kulipia baadhi ya madeni madogo ambayo nilikuwa nimekopa  hapo awali. Naishukuru mno BimaMkononi,” alisema Nyalufujo kwa furaha.
Kwa mujibu wa Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin huduma ya BimaMkononi imetengenezwa makusudi  kutoa bidhaa za Bima kwa Watanzania wote ambao wanaihitaji  ambao vinginevyo wasingeweza  kumudu huduma hiyo.
“Mteja anaweza kwenda  kujisajili hospitali yoyote  kwa vile hatuweki kizuizi  cha hospitali gani mteja anaweza kutumia- tutayafanyia kazi madai wanapotutumia taarifa sahihi (taarifa ya kuruhusiwa kutoka, taarifa ya madai ya hospitali, fomu ya madai ya bima iliyosainiwa). Kitambulisho cha mteja ni  ni namba yake ya simu na anaweza kujisajili kwa  kutumia namba *148*15#,  huduma  hii inafikia wateja kupitia simu za mkononi kusaidia  kufikiwa kwa urahisi  kadri inavyowezekana  kwa wakazi wa  mjini na vijijini. Bima Mkononi  hadi sasa imekuwa na matokeo makubwa  katika kusukuma mbele  kujumuishwa kifedha ndani ya  sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania  kuzifikia  huduma  za bima wanazozimudu  kutoka ndani ya simu zao.”
Tom Chaplain  alieleza kuwa  huduma hiyo imetengenezwa  mahsusi kwa  kuwapatia watu wote bima za maisha, afya na huduma binafsi ya ajali  ambazo zinaweza kuzisaidia  familia zao  kusimamia madhara ya kifedha ambayo yanaweza kusababishwa na matukio yasiyotarajiwa.
Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanapoel  alisema kwamba ushirikiano huu wa Tigo na Milvik katika kutoa huduma  hii ni moja ya mkakati wa Tigo katika kuendeleza mageuzi ya kidijitali  na kuendelea kuongoza katika kutoa huduma za kibunifu na zenye ubora wa hali ya juu kuwezesha BimaMkononi kupatikana kwa kutumia TigoPesa.
“Huduma hii imekuwa ni fursa kubwa kwa wateja wa Tigo kuifikia bima kwa urahisi kwa sababu BimaMkononi  inalenga kuwapatia Watanzania  njia mbadala wanayoimudu katika bima ya afya na maisha,” alisema Swanepoel.
Kujisajili kwa ujumla wanachokihitaji wateja kufanya ni  kupiga *148*15# na kufuata maelekezo.  Kudai piga namba: 0659071001 na tutakusaidia namna unavyoweza kufungua madai. 
 Mwisho

No comments: