Monday, April 3, 2017

Benki ya EXIM yapata faida ya bilioni 83.6


Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kushoto ni Mkuu wa kitengo cha fedha msaidizi wa Benki hiyo Issa Hamisi  na mwengine ni  Meneja Mkuu fedha Joseph Mrawa
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda akisisitiza jambo kuhusu na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Meneja Masoko wa Benki ya Exim Abdulrahman Nkondo (aliyesimama), akitoa utambulisho kwa waandishi wa habari viongozi wa Benki hiyo waliohudhuria hafla hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Msaidizi wa Benki ya Exim, Issa Hamisi akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda akitoa maelezo ya kina kwa waandishi wa habari kuhusu na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kushoto ni Mkuu wa kitengo cha fedha msaidizi wa Benki hiyo Issa Hamisi.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Msaidizi wa Benki ya Exim, Issa Hamisi  Seleman Ponda akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kulia  ni Meneja Masoko wa Benki ya Exim Abdulrahman Nkondo katikati ni Mkuu wa kitengo cha fedha msaidizi wa Benki hiyo Issa Hamisi.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Msaidizi wa Benki ya Exim, Issa Hamisi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.

Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kulia kwake ni Meneja Mkuu fedha wa Benki hiyo Joseph Mrawa.

Aprili 3 2017, Dar es Salaam

Benki ya Exim imepata faida ya Tsh bilioni 83.6 (kabla ya kodi) kwa mwaka wa fedha 2016 ikiwa imejumuisha faida ya Tsh bilioni 46.4 ya kuuza hisa ilizowekeza. Faida itokanayo na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kibenki ni Tsh 37.2 Bilioni.

Mapato yatokanayo na riba yaliongezeka kwa asilimia 25 mpaka Tsh 90.9 bilioni, ikiwa imechangiwa na ongezeko la mikopo pamoja na mkazo katika amana zenye riba nafuu.

Aidha katika kipindi hicho hicho, mapato yatokanayo na tozo mbalimbali za huduma za kibenki yaliongezeka kwa asilimia 14 mpaka Tsh bilioni 35.7 ukilinganisha na Tsh bilioni 31.3 kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ufanisi kwenye utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.

Faida hiyo imeongeza mtaji wa benki kufika Tsh bilioni 227 na kuongeza uwezo wa benki kuweza kufanya miamala ya kibiashara mikubwa zaidi.

Katika kuongeza uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wateja na kujiandaa kwa ukuaji wa kasi, Benki ya Exim imetelekeza miradi mbalimbali ya kiteknolojia.

Nina furaha kubwa kuwataarifu kwamba kati ya miradi 8 ya kiteknolojia, miradi 7 imemalizika kwa mafanikio”. Alisema Afisa Mkuu wa fedha wa benki hiyo Bw. Selemani Ponda na kusisitiza kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia, benki itaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.

Utekelezaji wa miradi hiyo kwaajili ya kubadilisha mifumo ya kiutendaji umepelekea uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu na teknolojia na hivyo kusababisha gharama za uendeshaji kupanda. Katika taarifa yake ya fedha jumla ya gharama ya uendeshaji ilipanda  kwa asilimia 24 hadi kufikia Tsh bilioni 99.

Benki ya Exim imejiandaa kuwahudumia wateja wa kada zote kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia wateja wote mara baada ya kutekeleza miradi ya kiteknolojia na kuongezeka kwa mtaji.


Akizungumzia mafanikio ya benki tanzu za Exim zilizopo katika nchi tatu: Komoro, Djibuti na Uganda, Bw. Ponda alisema kuwa Komoro na Djibuti wamefanya vizuri na kuweza kupata faida mara 3 ya mwaka uliopita na kufikia Tsh bilioni 8 kutokana na ukuaji mzuri wa uchumi na huduma bora. Na benki tanzu mpya ya Uganda ilipata hasara ndogo ya Tsh milioni 177, na inategemewa kufanya vizuri zaidi mwaka huu baada ya kuteleza mikakati mipya baada ya Benki ya Exim kununua hisa zaidi ya 58.6%.

No comments: