Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa hafla
maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys
inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 17 nchini Gabon. Fainali hizi zitafanyika kufanyika kuanzia Mei
14 hadi 28, 2017.
TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia timu
hiyo kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa
namba 22 33 44 pia kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki
ya Diamond Trust (DTB).
Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla maalumu
ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi maana lengo ni
kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo itafanyika kwenye
Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.
TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa makundi
mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi.
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi
ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba wawakilishi wa
makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya michango hii
wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni
rasmi katika hafla hii.
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz,
kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767
ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.
Aidha wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali,
mashirika ya umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao
pia tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao siku
hiyo ya Ijumaa.
TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Serengeti Boys
……………………………………………………………………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment