Umoja wa vijana wa
Chama cha Mapinduzi (UVCCM) leo umefanya mkutano na waandishi wa habari lengo
likiwa ni kujadili mustakabadhi wa nchi yetu na mambo mbalimbali yanayohusu
umoja huo.
Uvccm wamepongeza jitihada mbalimbali
zinazofanywa na serikali kwa kuweza kudumisha muungano. Lakini pia wamepongeza
wananchi wa pande zote mbili ikiwemo Tanzania bara na Tanzania Visiwani kwa
kuendelea kuenzi muungano huo tangu hapo mwaka 1964 mpaka hivi sasa. Ikiwa kuna
mataifa mengi yalijaribu kuungana lakini muungano wao haukuweza kudumu na kwetu sisi ni jambo la kujivunia kwa hivi
kesho kutwa kuweza kutimiza miaka 53 ya muungano huo. Lakini pia wametoa
wito kwa vijana wa Dodoma na maeneo ya karibu
kuondoa tofauti ya vyama na usiasa na kujitolea kuungana kushiriki
katika maadhimisho hayo ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya taifa letu
kuweza kufanya maadhimisho katika mji wa
Dodoma. Inafaamika kuwa UVCCM ni jiko pia ni
tanuru linalowapika vijana kuja kuwa warithi wazuri wa selikali na kisiasa.
Kufuatia hili umoja huo umeweza kufanya mabadiliko ya baadhi ya nafasi kutokana
wakuu wa idara wengine kuweza kuteuliwa kuwa makatibu wakuu CCM wa wilaya hivyo
kuacha baadhi ya nafasi wazi. Kamati ya utekelezaji UVCCM taifa ilikutana
katika kikao chake kilichofanyika upanga Dar es salaam tarehe 18/4/2017 iliweza
kuteua wajumbe wake kama ifuatavyo.
Doris H. Obeid – idara
ya uchumi uwezeshaji na fedha
Daniel M. Zenda – Idara
ya vyuo na vyuo vikuu
Jokate U. Mwegelo – Idara
ya uamasishaji na chipukizi
Mohamedi A. Abdalah – Idara ya organization, siasa na
uhusiano wa kimataifa
Islael sostenes - Idara ya usalama na maadili
Pia umoja huo umekemea vikali kitendo kinachofanywa
na gazeti la Tanzanite kupitia machapisho yake ikiwa la tarehe 10 – 16 lenye
kichwa kinachosema “UVCCM isafishwe “ na toleo lake la tarehe 24 – 30 lenye
kichwa ” kashfa nzito UVCCM “ umoja huo
wa vijana unamuomba muhariri wa gazeti hilo kuomba radhi mapema kabla hatua
stahiki hazijachukulia dhidi ya gazeti hilo kwani kitendo hicho ni kudhalilisha
umoja wa Vijana CCM na kuwafanya wananchi wasiwe na imani na umoja huo.
No comments:
Post a Comment