Monday, April 10, 2017

KCB BANK TANZANIA MWENYEJI TAMASHA LA 2JIAJIRI MALKIA WA NGUVU DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akizungumza na wanawake wajasiriamali 1,500 waliohudhuria hafla ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu. Naibu Waziri aliipongeza Benki ya KCB kwa kutambua mchango wa mwanamke katika jamii na kuanzisha program ya KCB 2jiajiri inayo lenga kutatua changamoto zinazo wakabili wanawake wajasiriamali Tanzania.

Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Mama Zuhura Sinare Muro akizungumza na wanawake wajasiriamali 1,500 waliohudhuria hafla ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji (wapili kushoto), na Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Mama Zuhura Sinare Muro (wa kwanza kulia) wakikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 6,000,000tsh iliyotolewa na benki ya KCB kwa Bi. Mwanaidi Mayowela na familia yake (waliokaa), kama tunu ya heshima katika kampeni ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu. Pamoja nao kwenye picha ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Bw. Masika Mukule (wapili kulia), Waziri wa Biashara na Viwanda- Zanzibar Mhe. Amina Salim Ally (watatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Kays Hygiene Products Bi. Hadija Idd Simba, (wanne Kulia), Mjumbe wa bodi ya benki ya KCB Bi. Fatma Chillo (watano kulia), mjumbe wa bodi ya benki ya KCB Bw. John Ulanga (wasita kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB Bi. Christine Manyenye.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji (wapili kushoto), akimpongeza Bi. Mwanaidi Mayowela (aliekaa kushoto) kwa kuwa mshindi wa kampeni ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu. Pamoja nao kwenye picha ni Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Mama Zuhura Sinare Muro (wa kwanza kulia), Waziri wa Biashara na Viwanda- Zanzibar Mhe. Amina Salim Ally (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Kays Hygiene Products Bi. Hadija Idd Simba (watatu Kulia), Mjumbe wa bodi ya benki ya KCB Bi. Fatma Chillo (wanne kulia), mjumbe wa bodi ya benki ya KCB Bw. John Ulanga (wa tano kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB Bi. Christine Manyenye. 

Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Bw. Ruge Mutahaba akizungumza na wanawake wajasiriamali 1,500 waliohudhuria hafla ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Bw. Masika Mukule akizungumza na wanawake wajasiriamali 1,500 waliohudhuria hafla ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu.

Waziri wa Biashara na Viwanda- Zanzibar Mhe. Amina Salim Ally akizungumza na wanawake wajasiriamali 1,500 waliohudhuria hafla ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB Bi. Christine Manyenye akizungumza na wanawake wajasiriamali 1,500 waliohudhuria hafla ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu.





Dar es Salaam, AprilI 6, 2017. Benki ya KCB Tanzania iliendesha tamasha la KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu jijini Dar es Salaam kwa wajasiriamali ambao ni wanachama wa KCB 2jiajiri pamoja na wasio wanachama. Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa King Solomon na kuhudhuriwa na wanawake wajasiriamali zaidi ya 1,500 ambao walisherehekea, kuonesha bidhaa zao na kuunda mitandao ya kibiashara ili kukuza masoko yao.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dr. Ashatu Kijaji, na Waziri wa Biashara na Viwanda – Zanzibar Mhe. Amina Salim Ally, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro na wajumbe wengine wa bodi ya KCB.
Akizungumza katika tukio hilo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Masika Mukule alisema kwamba “Hafla ya KCB 2jiajiri ni muendelezo wa programu ya KCB Bank kuwawezesha wanawake wajasiriamali (women empowerment/capacity building) ambayo ilizinduliwa rasmi Desemba, 2016, ambapo    hadi sasa tumewapa stadi za biashara endelevu wanawake 258 kutoka mikoa 6, ambayo ni Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Morogoro na Zanzibar, na tunaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara.”
 “2JIAJIRI” inalenga kuondoa vikwazo  vinavyowakwamisha wanawake  kama vile haki ya kumiliki mali,  kuanzisha ajira na sheria na kanuni  ambazo zimewakwamisha wanawake  dhidi ya manufaa, biashara endelevu na maisha yaliyoboreshwa. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na Kituo cha Ushindani na Ujasiriamali Tanzania (TECC) ambapo inawezesha wanawake wanaoshiriki kujitegemea, kuwa huru kiuchumi na kudhibiti ustawi wao kiuchumi na kijamii,” Mukule alifafanua.
“Mradi huu upo katika mkondo wa sera yetu ya benki ya uwekezaji kijamii ambayo inatoa kipaumbele kujihusisha kijamii kuliko endelevu lengo lake kuu likiwa ni kunyanyua maisha ya jamii,” alisema Mukule
Mukule alibainisha kuwa Benki ya KCB kimsingi inatambua mchango mkubwa wa wanawake wanaoutoa katika sekta binafsi hususani katika Ujasiriamali mdogo na wa kati (SMEs) na kuongeza kuwa  shughuli zao zinakumbana na  changamoto nyingi pamoja na upatikanaji wa mtaji, ufahamu finyu wa mambo ya kifedha, Utunzaji wa kumbukumbu za kifedha, Kufikiwa na huduma za kifedha, Sera ongozi za biashara na upatikanaji wa masoko
Mukule aliongeza, “Hivyo Lengo letu kwa ujumla ni kuwezesha wafanya biashara wanawake wa Kitanzania kuandaa mikakati ambayo inaboresha stadi zao na uwezo hivyo kuunda fursa nyingi za kibiashara kwa ajili yao.”

Wale wanaofanikiwa kuhitimu Programu ya KCB 2JIAJIRI wanapata fursa ya kipekee ya kujiunga na Klabu ya Biashara ya KCB ambayo inawaunganisha na jumuia za kibishara za kitaifa na kimataifa. Kadhalika wananufaika kwa kupata huduma ya washauri watatu katika nyanja za Kifedha Kisheria na Masoko kwa kuwapatia ushauri wa kibishara na kitaalamu.

No comments: