Friday, April 7, 2017

MDAHALO KUHUSU NAFASI YA DIASPORA KATIKA UCHUMI KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Bw. Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mdahalo wa Diaspora kuhusu uchumi na maendeleo ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam. 
Mratibu wa Vikoba Kimataifa Bw. Mwinyirwaka Hatibu akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mdaharo wa Diaspora kuhusu uchumi na maendeleo ya Taifa mapema leo jijini dar es salaam.  

Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia uongozi wa Ikolo Investiment LTD wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu mdahalo wa Diaspora leo jijini Dar es Salaam. 

Picha na Frank Shija – MAELEZO.WATANZANIA waishio ughaibuni (Diaspora ) wanatarajia kufanya kongamano la Uchumi litakalofanyika April 11 na 12,Mwaka huu kujadili fursa na changamoto za Tanzania kuelekea uchumi wa kati. 


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Magid Mjengwa alisema kongamano hilo litawezesha kubadilishana uzoefu kwa watanzania hasa zinazopatikana nchi wanazoishi. 

Alisema pia itafanyika mijadala ya namna bora ya kupata ruzuku kutoka katika asasi za nje zizazotoa misaada kwa jamii. 
"Kutakuwa na mijadala ya upatikanaji wa masoko ya bidhaa na mazao ya Tanzania katika nchi wanazoishi "alisema Mjengwa. 

Alisema katika mijadala hiyo pia wataongelea suala uwekezaji wa diaspora nchini na michango yao kwa taifa. 
" Tutajadili pia ni namna gani Tanzania inawatumia Diaspora katika kuleta mawazo mapya ya kuijenga na kuipeleka nchi katika uchumi wa kati kama zilivyofanya nchi nyingine kama Kenya na Ethiopia, " alisema Mjengwa. 

Naye Katibu wa kamati hiyo, Mwinyi Mwaka ambaye ameishi Italia kwa miaka 15 alisema kuna fursa nyingi katika masoko ya nje  hasa ya Ulaya kuhitaji mazao ya chakula. 

" Italia kuna 'supermarket' nyingi zinazohitaji matunda na mazao mengine ya chakula lakini kwa kuwa watanzania hawajui namna ya kulifikia soko hilo ni vema tukutane tujadili tutalifikiaje, "alisema Mwaka. 
Mwisho

No comments: