HABARI ZA KIJAMII

MEYA DAR ATAKA VIJANA WAJIRIWE KWA WINGI TAASISI YA MWALIMU NYERERE FOUNDATION


 Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita ameuomba uongozi wa Taasisi ya The Mwalimu Nyerere Foundation Square kuwaajiri vijana wa kitanzania kwa wingi katika taasisi hiyo pindi jengo hilo litakapokamilika ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamezungumzwa leo hii na meya wa jiji hilo wakati akifanya ukaguzi wa maendeleo katika jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Square.

Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia nchi kuwa na uzalendo wa kutoa ajira zaidi kwa vijana  pamoja na ongezeko kubwa la wageni katika Jiji hilo.

"Nachowasihi tu msisahau kuwaajili watoto wetu wa kitanzania takribani watanzania 300 hadi 400 wanaweza wakapatika, lengo lenu litafanikiwa kama mtaiimarisha misingi yenu mliyoanza nayo tangu awali"amesema

Pia ameuomba uongozi wa taasisi hiyo kufungua maktaba katika jengo hilo na kuzalisha vitabu  mbalimbali vinavyohusu hayati mwalimu Nyerere ambavyo vitawawezesha watanzania kupata kumbukumbu kwa urahisi na kuacha  dhana ya kwenda mkoani Musoma kutalihi.

"Kwa kuwa jengo hili ni kubwa  lipo karibu na bandari na linavutia, mkijitahidi kuweka vitu vinavyomonesha mwalimu moja kwa moja tutapata watalii wengi kutoka nje na kuja hapa nchini" amesema

Aidha amesema kupitia jengo hilo  la kisasa katika jiji lake
litachangia kwa kiasi kikubwa cha wageni kuja hapa nchini na kutalii na kuiingizia kipato nchi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku amesema jengo hilo litakuwa na sehemu mbalimbali ikiwemo hotel ya kisasa, taasisi ya mwalimu itakayokuwa na square mita 5800 pamoja
na Chuo .

Butiku amesema jengo hilo litakapo kamilika litakuwa chini ya kampuni ya ujenzi ya Estate LTD ndani ya miaka 40 na wao watabaki  kuiangalia taasisi pekeyake.

Meneja mradi wa kampuni ya CRJE Thomas Lee amesema jengo hilo lipo karibuni kumalizika na litakuwa la kipekee zaidi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.