Sunday, April 30, 2017

MH. MWAKYEMBE KUZINDUA KITABU CHA COLOR OF LIFE DAR ES SALAAM

Waziri wa sanaa utamaduni na michezo MH Harrison Mwakyembe amezindua kitabu kilichobeba jina la THE COLOR OF LIFE kilichoandikwa na muandishi wa kitanzania Ritha M. Tarimo. 

Uzinduzi huo umefanyika kwenye hotel ya HYATT REGENCY jijini dar es salaam tarehe 30 ya mwezi march 2017. MH. Mwakyembe aliweza kupongeza jitihada za dhati zilizofanywa na dada huyo na kusema kuwa yeye ni shujaa na ni mfano wa kuigwa na jamii.  

Alisema  ni ngumu sana kwa nchi kama yetu ya Tanzania ambayo vijana wake wengi wameweka akili zao kwenye mitandao kuweza kujitokeza mtu kuandika kitabu. sisi kama viongozi  inabidi tumpe moyo na kuweza kurudisha utamaduni wa zamani wa kusoma vitabu “Kwani leo hii ukienda maktaba ukiona vijana wapo wengi jua kuna mtihani karibu” alisema . 

Aliongezea kuwa amekisoma kitabu hicho japo sio mpaka mwisho lakini akuona makosa  na kimeandikwa vizuri. Muandishi amejaribu  kuwatia moyo vijana kuwa wanapotafuta kitu wasichoke mpaka wakipate. Na hii itafanya nchi yetu kusifika kuwa hata sisi tunawez kuandika vitabu vyetu kwa kiingereza.

WAZIRI WA SANAA UTAMADUNI NA MICHEZO DKT HARRISON MWAKYEMBE AKIONGEA NA  WAGENI WAALIKWA HYATT REGENCY DAR ES SALAAM

Ritha Tarimo ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho alisema yeye kwa nafasi yake alihitaji kutengeneza historia kupitia uandishi wa vitabu kama ilivyo kwa wengine walivyoweza kuweka nguvu kwenye muziki, mpira, siasa nk. Na sababu kubwa iliyomfanya kuandika kitabu hicho ni kuweza kuwasaidia wanafunzi ngazi ya sekondari, vyuoni ili waweze kugundua mapungufu yake ili na wao waje kuwa waandishi wazuri zaidi yake . Lakini pia aliweza kuona ni vyema kutumia lugha ya kiingereza kwa kuwa shule zote kuna somo la hilo. Na vitabu vingi vinavyofundishiwa ni vya kutoka nje ambao waandishi wake ni watu wa mataifa mengine. Ivyo basi yeye aliamua kujikita huko kuweza kuwapa moyo waandishi wengine wa kitanzania waweze kufanya kama yeye alivofanya ili taifa liweze kupata vitabu vitakavyotumika kwenye mitaala ya shule zetu.

RITHA M. TARIMO AKITOA UFAFANUZI JUU YA KITABU CHAKE KINACHOZINDULIWA NA WAZIRI MWAKYEMBE

Lakini pia aliweza kumshukuru MH. Halisoni mwakyembe kwa kuweza kukubali wito wake wa kuhudhulia kwenye tafrija hiyo na kuweza kupongeza kile alichokifanya. Na kumuahidi kununua nakala kadhaa  za  kazi yake.  kwenda kuwaonyesha na viongozi wenzake wa ngazi ya juu kama waziri wa elimu na wengine ili kuweza kuwapa motisha vijana wengine wenye vipaji kama vyake. pia aliweza kuishukuru familia yake pamoja na marafiki kwa mchango wao wa dhati wa kimawazo hata kiuchumi kwa kuweza kufanikisha kwa uzinduzi huo.

MH. HARRISON MWAKYEMBE AKIKATA UTEPE KUZINDUA RASMI KITABU CHA THE COLOR OF LIFE

BAADA YA KUKATA UTEPE MH. MWAKYEMBE NA RITHA TARIMO WAKIONYESHA WAGENI WAALIKWA KITABU KILICHOZINDULIWA

PICHA YA PAMOJA BAADA YA TAFRIJA KUISHA

PICHA/STORY NA MUANDISHI WETU VICENT MACHA.

No comments: