Monday, April 10, 2017

ROMA AFUNGUA MJADALA UPYA,KUTEKWA KWAKE,AELEZA KIDUCHU,WENGI WAHOJI USIRI WAKE


Anaeongea kwa sasa ni msanii Roma na anatoa shukrani kwa wote bila kujali itikadi zao, anasema kilichowapata watu wafanye kama case study.

Roma anasema hawana uhakika wa usalama wao hata kidogo, amesema nature ya tukio, studio zilizopo Tongwe records yuko tangu 2007 na ni eneo salama sana. Amesema wana majirani wanaowapa amani sana ikiwemo ujirani na Tibaigana, Waitara na mstaafu mmoja wa Magereza.

Amesema hofu hiyo isiishie kwao kwani inaweza ikarudi kwa yeyote muda wowote, mtu yeyote inaweza kumkuta. Amedai wao ni wachanga mno na hawawezi kupambana na yeyote. Anasema Bin Laden hayuko sawa na anastuka sana mpaka kuwastua watu wote.

Amedai kuna watu wanaamini hakuna kilichotokea kwa kudhani ni kiki na wengine wanasema wanatumika kisiasa labda kuchafua serikali.

ROMA: Tunatafuta ruzuku yetu kupitia mziki, tumelia sana kwa haya maneno tena mengine kutoka kwa watu wa karibu sana ikiwemo wanamuziki, si kweli. Tunaishi familia za kawaida na hatuwezi kurisk maisha yetu kwa ajili ya hela au sababu nyingine yeyote.

Kilichotokea ni kweli, nadhani mnaona mwili wangu(anaonyesha), linatuumiza sana mtu kusema tumepewa dola 5,000. Tumeumia, tumepigwa kiukweli na tumeripoti kwenye vyombo vya dola.

Sheria zetu zinasema jambo likianza uchunguzi ni njema kulielezea kwani wanasema linaharibu upelelezi.

Nilifika Tongwe na kuwakuta wenzangu, haikupita nusu saa wakaja watu na silaha za moto na amri ilikuwa kuingia ndani ya gari, tukiwa tumefungwa usoni na pingu, ilikuwa Jumatano jioni na tumekuja kupata usalama tumekuja kuupata Ijumaa jioni na kulikuwa na mahojiano yanaendelea yakiambatana na vipigo. Maojiano hayo ndo hayo temsharipoti.

Tulifungwa tena na kuachwa eneo ambalo hatulijui tukatupwa kwenye dimbwi la maji, tukajikuta tuko salama na baada ya kutembea sana tukakuta kibao kimeandikwa Mahaba beach na kugundua tulikuwa Ununio.

Swali: Mlingundua mlitupwa beach, mlienda beach Oysterbay police

JIBU: Ilikuwa ni usiku, baada ya muda tulipogundua Ununio, nilikuwa na madoa ya damu. Mpaka mtu ujue mimi ni Roma ilikuwa ngumu, tulifika hadi Kunduchi na kukuta boda sita na kumuomba Moni aite boda, tukaenda hadi nyumbani Mbezi, kuingia ndani hamna mtu, nikawaambia wenzangu tubadili nguo, ilikuwa inaelekea Alfajiri, mtu wa bajaji tukamuomba simu kumpigia bosi wetu.

Tulipofika alikuwa tayari amempigia Ruge Mutahaba, walikuwepo na waliumia sana, wao ndio wakatupa way forward na kusema walifungua hii kesi kituo cha polisi hivyo tukaenda kituo cha polisi Oysterbay.

SWALI: Waliwaachia masharti yoyote

JIBU: Ipo ndani ya upelelezi.

SWALI:Chanzo kilikuwa mziki wako?

JIBU: Siwezi kujua, upelelezi unaweza kuleta majibu.

Dada anaeonekana muongozaji anasema hamna swali jingine na anamkaribisha waziri Mwakyembe.

Mwakyembe: Pale ambapo kuna tatizo na msanii yeyote nitaarifiwe kwanza mimi waziri mwenye dhamana, wasanii wote ukihojiwa na mtu usiemjua wa ajabu nitafute, niliposikia taarifa hii nikajiuliza chombo cha dola kimekiuka tena taarifa yangu? Hili ni swala scientific tuache kupiga ramli, wenzetu wamesema tuwaache wafanye upelelezi, hii sio hali ya kawaida

Inaweza kuwepo wasanii(sio wanamuziki) wachache wanataka kutuvuruga, nawashukuru sana.

SWALI: Bashe amesema vyombo vya usalama vimehusika

JIBU: Umeleta maswala ya kina Bashe, mimi hapa Mwakyembe, mambo hayo yako bungeni.

Swali: Kuna mtu alisema Roma ataonekana kabla ya Jumapili na kweli akaonekana

Moderator: Sasa tuishie hapohapo.

Mwakyembe: Mkiendelea kupiga kelele kama watoto wa shule naondoka hapa, wewe unaamini ni vyombo vya dola? Siwezi kuamini mpaka nione ya recording ya huyo kiongozi.

No comments: