BIASHARA

Uber Tanzania yatangaza kuunga mkono Dereva- Washirika kwa uzinduzi wa kituo kipya cha huduma cha Greenlight Hub kinachofunguliwa Dar es Salaam


Inline image 1

Inline image 2
Taarifa kwa vyombo vya habari

Uber Tanzania yatangaza kuunga mkono Dereva- Washirika kwa uzinduzi wa kituo kipya cha huduma cha Greenlight Hub kinachofunguliwa Dar es Salaam

Dar es Salaam, April 5 2017… Uber Tanzania walitangaza ufunguzi wa ofisi mpya za kuwasaidia na kuwaimarisha maelfu ya dereva-washirika wanaojikimu kupitia Uber mjini Dar es Salaam.


Ofisi hizi mpya zenye nafasi kubwa, zipo katika jumba la Viva towers, gorofa ya 1, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Road ni nafasi ya ofisi ya kisasa kabisa iliyopewa jina la ‘The Greenlight Hub’ mahsusan kwa ajili ya kuwahudumia dereva-washirika wa Uber kama kituo nyenzo ambako wataweza kutafuta msaada wa kiufundi wa uendeshaji au kuuliza maswali kuhusu programu hii ya Uber.

Akizungumza katika sherehe hiyo ya uzinduzi, Kiongozi wa Uber nchini Tanzania Alfred Msemo alithibitisha kuwa kituo hicho kipya kitawezesha Uber kuwa na fursa ya kuwasaidia hata washirika zaidi na kupunguza muda unaochukuliwa na dereva wanaposubiri kuwaona mwakilishi wa Uber. “Napenda kuwashukuru wanachama wa kundi letu la kuwahudumia dereva-washirika kwa kutekeleza kazi yao kwa bidii ili kutoa usaidizi bora zaidi kwa kila dereva-mshirika wetu”.

Kama kuwashangaza na kuwafurahisha dereva-washirika waliohudhuria sherehe hiyo ya kukata utepe, Uber pia waliwatambua na kuwazawadi kwa vocha za kununua bidhaa  Nelson Wallace,  Said Salmin na Mohamed Juma ambao ndio dereva-washirika waliokamilisha safari nyingi zaidi na kufikia viwango bora mtawalia.   Vile vile walimtambua na kumtunuku kwa zawadi Margareth Kiondo dereva-mshirika aliyefikia kiwango cha juu cha ubora na aliyekamilisha safari nyingi zaidi pamoja na Anthony Matiku ambaye ndiye dereva aliye na idadi kubwa zaidi ya kuwajuza wateja.  

Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki wa Uber, Loic Amado, ambaye aliangazia zaidi azimio la uzinduzi wa kitovu cha huduma cha Greenlight Hub kuwa ulichochewa na haja yetu ya kutaka kuwasaidia na  dreve-washirika wetu amabo wanaongezeka idadi kila kukicha. Kituo hiki cha Greenlight Hub ambacho awali kilikuwa katika jumba la Muccadam barabara ya upanga, kilihudumia dereva zaidi ya 200 kila wiki. “Nafasi hii mpya ya ofisi inahusu hasa utoaji huduma bora zaidi za haadhi ya kimataifa kuwasaidia maelfu ya dereva-washirika wanaoendesha usafiri wa Uber jijini Dar es Salaam. Eneo hili letu jipya limeimarishwa ili kufanikisha na kustawisha ukuaji na kupatia kasi juhudi za kushughulikia mahitaji ya washirika wetu, kutuwezesha sisi kutoa thamani bora ya kipekee na huduma zisizo kifani” alisema Amado.

Kituo cha Greenlight Hub kitakuwa wazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa Tatu asubuhi hadi saa kumia na moja jioni,  na kutakuwa muda mfupi wa kusubiri, nafasi ya kutosha ya kuegeshea magari  ya dereva-washirika wetu na vyumba maalum vilivyotengwa kuwahudumia dereva waliyo na mahitaji maalum kama vile ulemavu. 
Kituo kipya pia kitawawezesha dereva-washirika kuwa na fursa ya kupata huduma ya moja ka moja kutoka wawakilishi kwa mpango wa suluhisho za gari wa Vehicle Solution Programme na watoaji huduma wengine mbali mbali jambo ambalo ni thamani ya ziada kwa dereva-washirika wetu kama vile watoaji huduma za simu, benki na watia huduma za kiufundi.The hub will also give technical support that will enable driver-partners give feedback of the services received. kitovu pia kinatarajiwa kutoa msaada wa kiufundi ambao utawezesha dereva-washirika kuleta  maoni yao juu ya huduma wanazopokea.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.