Tuesday, May 23, 2017

Breaking News-VIDEO CHAFU-Mshauri wa ACT WAZALENDO,Wakili Msando Ajiuzulu Rasmi

NDUGU ALBERTO MSANDO AJIUZULU USHAURI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO


Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.

Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu  "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka".

Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.

Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. 

Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo 
Dar es salaam mei 23, 2017

No comments: