Sunday, May 28, 2017

KAMANDA SIRRO KUCHUKUA NAFASI YA ERNEST MANGU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo May 28 2017 amemteua Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP). Kabla ya Uteuzi huo IGP Simon Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa kesho Jumatatu tarehe 29 May, 2017 saa 3:30 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments: