Kituo cha sharia na haki za binadamu nchini LHRC leo tarehe
12 mwezi mei kimekutanisha wawakilishi wa vyombo vya habari ikiwa ni waandishi
pamoja na wahariri. Lengo likiwa ni kuhamasisha uhuishaji wa katiba mpya.
Semina hiyo iliyofanyika hotel ya Seashells Millenium tower jijini Dar es salaam iliongozwa na muadhiri wa chuo kikuu Prof. Khoti Kamanga akitoa
mchanganuo kuhusiana na mchakato wa
katiba ulivyoanza na mpaka ulipokwama.
Prof. Khoti Kamanga akitoa ufafanuzi juu ya katiba ya mwaka 1977 |
Akitoa mawasilisho katika semina hiyo Prof Kamanga alipongeza
jitihada za Rais wa awamu ya nne DK Jakaya Kikwete kwa kuweza kugundua kuwa
katiba yetu ina mapungufu hivyo tunahitaji katiba mpya.
Hivyo basi mwaka 2011 aliweza kuunda baraza makini kwa
ajili ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya. Japo kuwa katiba iliyopatikana kutokana na
maoni ya wananchi haikuweza kupewa nafasi lakini Rais alionyesha moyo wa
kuitaka katiba mpya ambayo ni dira ya watanzania.
Waandishi wa habari pamoja na wahairi wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mjadala |
Prof Kamanga alisema kuwa sote tunafahamu kuwa katiba iliyopendekezwa
haina tofauti sana katiba ya mwaka 1977 kwa kuwa zote zina mapungufu. Na miongoni
mwa mapungufu hayo ni kumpa Raisi madaraka makubwa, na pia kuna kifungu
kinachosema katiba ikijadiliwa bungeni ikashindikana kufikia muafaka basi
inabidi itumike katiba ile ile yenye mapungufu. Lakini pia kingine ni kero za
muungano ambazo bado hazina muafaka.
Waandishi wakiwa bize na kazi |
Katiba ni chombo kinachotumika kwa watu wote hivyo basi
inabidi ikubalike na pande zote sio kundi dogo la watu ndio likubali na wengine
wapinge inakuwa sio katiba ya kufuata haki.
Katika semina hiyo yameweza kutolewa mapendekezo mbalimbali
ikiwemo kuwa na ukomo wa wabunge wasiweze kuongoza zaidi ya awamu mbili. Lakini
pia baadhi ya mambo yasiamuliwe bungeni mpaka wabunge waje kuomba Ridhaa kwa
wananchi juu ya jambo husika.
Mbunge anapokosea au wananchi wameona mbunge wao hafai
waende kuomba ridhaa kwa spika avuliwe nafasi yake. Lakini lingine mbunge
asipewe nafasi ya uwaziri mbunge awe kama mbunge na waziri awe waziri ili
asiweze kupewa feva kwenye baadhi ya mambo yake.
Waandishi wa habari wakiendelea kufuatilia mjadala |
Katiba iweze kuboreshwa iwe ndogo kiasi kwamba hata kwenye
mfuko wa suruali iweze kuingia isiwe mzigo mkubwa mpaka mtu aone uvivu kubeba. Na
baadhi ya vifungu vitolewe vijadiliwe bungeni vibaki kama sheria ili kupunguza
mlolongo mrefu wa vifungu.
Waandishi wa habari na wahariri wametakiwa kutangaza,
kuchapisha machapisho na kutengeneza vipindi vinavyo hamasisha udaiji wa katiba
mpya. Pia wameshauriwa kutochoka japo kuwa ni kazi ngumu na kutoogopa kudai
katiba mpya kwani ndio msingi wa haki zote.
Waliweza kumshauri Raisi wa awamu ya tano DK. John pombe
magufuli kuweza kurejesha tena mchakato wa katiba mpya kwani ndio kiu ya
watanzania kwa sasa.
Prof.Khoti Kamanga akiendelea kutoa hoja |
No comments:
Post a Comment