Friday, May 5, 2017

KUTANA NA SIDIRIA 'BRAZIA' YENYE UWEZO WA KUGUNDUA SARATANI YA MATITI

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Mexico ameshika headlines duniani baada ya kutengeneza sidiria ‘Brazia’ ambayo ina uwezo wa kugundua saratani ya matiti katika hatua za mwanzo,Teknolojia hii ya kugundua saratani kwa haraka na ufanisi imetajwa kuwa ya kwanza kuwahi kutengenezwa na mtu yoyote duniani.

Julian Rios Cantu, 18, ametajwa kuwa mjasiriamali mgunduzi mdogo zaidi duniani kuwahi kutengeza sidiria ambayo imewekwa kifaa maalum ambacho kina uwezo wa kupima hali ya joto na mtiririko wa damu katika matiti, hivyo kuweza kuonesha dalili za ugonjwa wa saratani ya matiti. 

Akizungumza na BBC Julian Rios Cantu amesema kuwa alisukumwa kutengeneza siridia hizo ili kuwa msaada kwa wanawake wote duniani baada ya mama yake kugundulika na ugonjwa wa saratani ya matiti. Sidiria hizi zimetabiriwa kupunguza athari zinazoletwa na ugonjwa wa saratani ya matiti kwa asilimia 70.
Juliana Rios Cantu mwenye umri wa miaka 18 ametengeza sidiria ambayo anasema itatoa onyo la mapema kwa mtu mwenye dalili za saratani hiyo.

Sidiria hiyo kwa jina Eva iliotengezwa naye na marafikize watatu walianzisha kampuni hiyo pamoja.

Lakini wamechangisha fedha ili kuifanyia majaribio na wiki hii wakashinda tuzo katika hafla ya wanafunzi wanaotaka kufanya biashara.

Kampuni yao Higia Technologies iliibuka mshindi baada ya kuzishinda kampuni nyengine za biashara kutoka kote duniani ili kushinda dola 20,000 kuzalisha wazo lao.

Uvimbe ulio na saratani unaweza kupandisha vipimo vya joto mwilini.Rais wa Mexico alimpongeza Julian kwa kushinda tuzo la wanafunzi wafanyibiashara.

Wazo la sidiria ya Eva ni kwamba ina sensa ambazo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kumuelezea kuhusu mabadiliko yanayomsumbua.

Wanawake wanaohitaji sidiria hiyo watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki ili kupata vipimo vya sawa.

Hii ni awamu ya kwanza ya dalili za ugonjwa huo.

Tayari sidiria hiyo imefanyiwa majaribio na itafanyiwa vipimo vyengine vya kimatibabu kabla ya wataalam wa ugonjwa wa saratani kuipendekeza kuwa njia ya kugundua saratani.


Anna Perman kutoka kituo cha utafiti cha Uingereza kimeambia BBC : Tunajua kwamba uvimbe huo una mishipa isio ya kawaida ya kupitisha damu na tunajua kwamba kasi ya damu katika mishipa sio thibitisho kwamba mtu anakabliwa na saratani. 

No comments: