Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alitoa kauli hiyo leo (Jumamosi) wakati akizungumza na wanahabari ofisi kwake Mikocheni.
Amesema amelaani kitendo hicho na kusema kongamano hilo halikuwa na nia mbaya bali lilikuwa limelenga kujadilia mambo mbalimbali kwa mustakabali wa Taifa.
“Nimesikitishwa na kitendo hiki na nimeshangaa kwa jambo hili halikemewi.Nchi hii ni moja na kila mtu ana haki.
“Walituzuia mikutano ya hadhara tumetii, tumeamua kufanya mikutano ya ndani wanatufuata fuata,”amesema Lowassa ambaye aliwahi Mbunge wa Monduli kwa nyakati tofauti.
No comments:
Post a Comment