Saturday, May 13, 2017

MEYA WA JIJI AZINDUA MICHUANO YA DRAFTI DAR ES SALAAM

Meya wa Dar es salaam Mh. Isaya Mwita leo tarehe 13 mwezi mei amezindua rasmi mashindano ya mchezo wa Drafti kwa jiji la Dar es salaam. Ufunguzi huo uliyofanyika katika uwanja wa mwembe yanga manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam Uliudhuriwa na mbunge wa Temeke Mh. Mohamedi Mtolea pamoja na wadau mbalimbali wa mchezo huo pamoja na washiriki toka kona mbalimbali za jiji Hilo

Meya wa jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita akiongea na washiriki pamoja na mashabiki wa mchezo wa drafti 

Akiwasilisha changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wachezaji wa mchezo huo mwenyekiti wa mchezo wa drafti kwa Jiji la Dar es salaam. Bw. Kiraba Ngibbombi alisema kuwa wanakabiliwa na tatizo la usajili huku meya angewasaidia japo chama cha wacheza drafti kiweze kutambulika kitaifa kama michezo mingine ikiwemo mpira wa miguu na mpira wa kikapu.

Kukosa ofisi na vitendea kazi ikiwemo kumpyuta, mashine za kuprinti karatasi pamoja na madrafti ni miongoni mwa changamoto zinazokikabili chama hicho.

Na pia  alimuomba meya kuwa kama itawezekana wakati mwingine. Mashindano yatakapo anzishwa waweze kupata japo chakula na  nauli kwa washiriki kwani  watu hao wanatoka kona tofauti tofauti za mji wa Dar.
Mwenyekiti wa mchezo wa Drafti Dar es salaam Kiraba Ngibbombi akitoa malalamiko yao kwa mgeni rasmi
Mstahiki Meya aliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo na kero zao kwa kuwa viko chini ya uwezo wake aliwaomba viongozi wa chama hicho baada ya kuwasaidia kuweza kupata usajiri waweze kutengeneza katiba na sharia nzuri. Ili kupanga mashindano yawe yanafanyika kila baada ya muda gani? kama ni kwa mwaka mara mbili au mara moja. 

Lakini pia waweze kupata timu kwenye kila wilaya ziweze kushiriki na kupata wataalamu wengi zaidi wa mchezo huo. Ili mashindano yatanuke kuwa ya taifa na hatimaye kuvuka mipaka kuwa ya kimataifa.
Mchezo wa kukata na shoka kati ya mstahiki meya wa Dar na mbunge wa Temeke
Baada ya uzinduzi huo ulianza mchezo wa kupimana nguvu kati ya mstahiki meya wa Dar es salaam Isaya Mwita  pamoja na mbunge wa Temeke Mohamedi  Mtolea. Na waliweza kucheza michezo mitatu na mstahiki meya aliweza kuibuka mshindi wa bao moja na michezo miwili waliweza kutoa sare hivyo kumfanya Meya Bw Isaya mwita kuibuka na ushindi.

Meya wa jiji kulia akiwa na mbunge wa Temeke

No comments: