Monday, May 29, 2017

MTANDAO WA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI WATOA TAMKAO KWA WABUNGE WANAOPINGA MABINTI WALIOPEWA MIMBA WASIRUDI MASHULENI.

Mwenyekiti wa mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania(TECMN) Valerie N. Msoka akiongea na waandishi wa habari leo mapema jijini dar es salaam kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Tamwa Bi. Edda Sanga.
Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania ‘TECMN’ umesikitishwa na kitendo cha baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunga mkono hoja ya kutowapa nafasi ya kuendelea na masomo wanafunzi wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni baada ya kujifungua.
Mwenyekiti wa TECMN, Valerie Msoka amesema kitendo kilichofanywa na Wabunge kinarudisha nyuma jitihada mbalimbali zinazofanywa katika kuleta usawa wa kijinsia na kumuinua mwanamke kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Aidha, ameongeza kuwa sababu mbalimbali zilizotolewa na Wabunge ni za kisiasa zaidi kwa kuwa hazizingatii ustawi wa mtoto wa kike na mustakabali wa maisha yake akisema Wabunge walioshabikia hoja hiyo wamedhihirisha kutotambua viini vya matatizo yaliyomokatika jamii.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria mkutano huo uliofanyika makao makuu ya kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC).

No comments: