Tuesday, May 30, 2017

NI KOSA KUMLISHA MTOTO CHAKULA KWA KIJIKO...


Watoto ambao hulishwa chakula kwa kijiko wameelezwa kuwa hatarini zaidi kuwa na uzito mkubwa au unene kupita kiasi ukilinganisha na watoto ambao wanakula wenyewe kwa mikono yao, kwa mujibu wa utafiti mpya.
Amy Brown, Professor katika Chuo Kikuu cha Swansea amesema kuwa watoto wanaopewa nafasi ya kula wenyewe kwa mikono yao huwa na uwiano mkubwa wa afya bora hivyo wazazi wameshauriwa kutowalisha kwa kijiko watoto wenye umri wa zaidi ya miezi sita kwa sababu wanakuwa tayari wanaweza kula vyakula vigumu.
Akiongea na Sunday Times mwandishi huyo wa kitabu cha Why Starting Solids Matters, ambacho kitachapishwa wiki ijayo amesema lazima watoto waruhusiwe kula kidogo au zaidi pale wanapojifunza kula wenyewe akidai kuwa kutumia kijiko huwafanya watoto kula zaidi ya wanavyohitaji

No comments: