Friday, May 5, 2017

NYANI ALBINO AOKOLEWA AKISHAMBULIWA NA WANAKIJIJI

Nyani mkubwa albino asiye wa kawaida anatunzwa na kundi moja la kuwalinda wanyama nchini Indonesia baada ya kuokolewa akishambuliwa na wanakijiji.

Nyani mkubwa albino asiye wa kawaida anatunzwa na kundi moja la kuwalinda wanyama nchini Indonesia baada ya kuokolewa.

Nyani huyo wa kike mwenye nywele nyeupe na macho ya buluu alikuwa anazuiliwa katika eneo moja la mashambani nchini Indonesia katika eneo la kisiwa cha Borneo.

Alikuwa amezuiliwa katika kizimba kidogo kwa siku mbili na bado alikuwa akionesha tabia za msituni kulingana na kundi hilo la kuwalinda tumbili la Borneo Orangutan Survival Foundation.

Mnyama huyo huenda akawachiliwa na kwenda msituni ,limesema kundi hilo.

Nyani Albino ni wachache na huyu ni wa kwanza kuchukuliwa na kundi hindi hilo katika historia yake ya miaka 25.Mnyama huyo alikuwa na damu iliokauka katika pua yake ishara kwamba huenda alipata majeraha alipokuwa akikabiliana na wanakijiji waliomkamata

Kundi hilo limesema kuwa limebaini kwamba mnyama huyo alikuwa na tatizo la albino baada ya kumfanyia ukaguzi likisema kuwa macho yake yalikuwa hayapendi mwanga mwingi.

Mnyama huyo anayeaminika kuwa na umri wa miaka 5 anachunguzwa katika kituo cha kubadili tabia cha shirika hilo, ambacho kinawahifadhi zaidi ya tumbili 500.

Tumbili hao wa Borne huorodheshwa kama wanaoangamia na shirika la kitaifa la uhifadhi wa asilia IUCN.

Idadi yao ilipungua kwa takriban asilimia 60 kati ya 1950 na 2010 kutokana na uharibifu wa mazingira yao na uwindaji haramu na kushuka zaidi kwa asilimia 22 kunatarajiwa kati ya 2010 na 2025, kulingana na shirika hilo.


Mnyama huyo alikuwa na damu iliokauka katika pua yake ishara kwamba huenda alipata majeraha alipokuwa akikabiliana na wanakijiji waliomkamata

No comments: