UCHUMI

SERIKALI YARIDHIA KUANZISHA MFUMO WA UAGIZAJI WA MBOLEA KWA PAMOJA (BULK PORCUREMENT SYSTEM)

Serikali kupitia Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) imeanzisha mfumo wa uwagizaji wa mbolea kwa pamoja(BULK PROCURENT SYSTEM) baada ya kujiridhisha kupitia kikosi kazi kilichoundwa na wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi ambacho kilifanya upembuzi na kukusanya maoni ya wadau kupitia vikao mbali mbali na kupata maoni toka kwa taasisi za serikali ambazo zimekuwa zikisimamia mfumo wa ununuzi wa petrol kwa pamoja kama EWURA,PBPA na FCC ili kupata uzoefu kuhusu mfumo huo.

Kimu Mkurugenzi Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) Bw lazaro kitandu akitolea ufafanuzi swala la ununuzi wa mbolea kwa pamoja na kulia ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano selikalini toka wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi bw Richard Kasuga.

Akitolea ufafanuzi huo leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo Jijini Dar es salaam,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Bw.Lazaro Kitandu amesema serikali kupitia Mamlaka hio imeanzisha mfumo huo ili kuimarisha utaratibu wa usambzaji wa mbolea ambapo wadau wote watapata uhakika wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani,pia itawawezesha wafanyabiashara wadogo kukua na kushiriki katika biashara ya mbolea.

Aidha ,Bw.Kitandu amesema kuwa wizara ya kilimo ilisha andaa kanuni za kusimamia ununuzi wa mbolea kwa pamoja  yaani Fertilizer (Bulk procurement)Regulation G/N NO.49/2017 ambayo ililindiwa na waziri mwenye dhamana kwa mujibu wa sheria ya mbolea Namba 9 ya mwaka 2009 kifungu cha 51 na kanuni zake za mwaka 2001,kuwa itatangazwa zabuni kwa ushindani(compitative bidding)na mfumo upo wazi kwa mtu yoyote kushiriki kwa kuzingatia taratibu za kanuni hizo.

Waandishi wa habari walioudhuria mkutano huo uliofanyika idara ya Habari maelezo mapema leo jijini Dar es salaam
"Kanuni za ununuzi wa mbolea kwa pamoja zinaelekeza kwamba uagizaji wa mbolea kutoka nje ya nchi lazima ufanyike kupitia utaratibu ulioainishwa ambao ni kwa kutangaza zabuni kwa ushindani(compitative bidding) na kwamba mfumo upo wazi kwa mtu yoyote kushiriki."alisema
Hata hivyo, mbolea ni moja ya kichocheo muhimu katika kuongeza uzalishaji wa mazao wenye tija na katika nchi kusini mwa jangwa la sahara Tanzania ni nchi mojawapo yenye matumizi ya chini ya mbolea ya kilo19 za virutubisho kwa hekta katika ngazi ya wakulima wadogo, kiasi hiki hakiendani na malengo ya azimio la nchi za SADC kufikia angalau kilo50 kwa hekta moja, na huku mfumo huu ukiwa utaanza kuagiza mbolea za aina mbili tu kwa msimu wa 2017/2018 yaani mbolea ya kupandia(DAP)na kukuzia(UREA)na mbolea zingine kufuatia baadae kadri itakavyoonekana mfumo huu umeleta manufaa kwa mlaji

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.