HABARI ZA KIJAMII

TGNP MTANDAO WAIJADILI BAJETI YA WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI 2017/18

Mtandao wa Jinsia nchini Tanzania TGNP leo Umeendesha warsha fupi iliyowakutanisha wanahabari na wanaharakati mbalimbali kujadili bajeti ya wizara ya maji na umwagiliaji ya mwaka 2017/18.

Akiongoza warsha hiyo Mr. Melkizedek Karol  alisema kuwa bajeti ya mwaka 2016/17 na 2017/18 kumekuwa na utofauti mkubwa sana kwa maana mwaka huu bajeti imeshuka kwa zaidi ya bilioni 200. Kwa mwaka jana  bajeti ilikuwa ni bilioni 915.1 kwenye mradi wa maendeleo  na kwa mwaka huu ni bilioni 623.6. na ikiwa imepanga 75% kwa pato la ndani na 25% pato la nje.

Na mwaka 2017/18 ikiwa miradi ya maendeleo 66% kwa kipato cha ndani na 34%kwa kipato cha nje kwenye mipango ya maendeleo ikiwa imepangwa kutumika 623.6 na wananchi wakiwa wanasubiri kuona kama kweli kiwango hicho kitatolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Melkizedek Karol akifafanua jambo kwenye semina iliyofanyika ofisi za TGNP mtandao mabibo Dar es salaam


Kwani mwaka uliopita wa fedha kulikuwa na mradi wa maji kutoka ziwa victoria kwenda shinyanga kahama na tabora uliotengewa bilioni 22.4 na badala yake kutolewa milioni 500tu.
Lakini pia serikali imeweza kuainisha mambo mambo mengine ya kufanyika kwenye bajeti yake ya maendeleo ya mwaka  2017/18 kama vipaumbele kwenye bajeti yake ya bilioni 623.6 na mambo hayo kama yafuatayo.

Ukamilishaji wa miradi 509 katika halimashauri mbalimbali na kuanza miradi mipya vijijini.

Kutekeleza miradi ya maji vijijini katika maeneo yenye ukame na shida  kama Dodoma ,singida pamoja na shinyanga (kishapu DC)

Kuendesha upanuzi wa miradi ya maji vijijini vijiji 100 kandokando ya bomba kuu la KASHWASA.
Kuendelea na ujenzi  na ukarabati wa mabwawa

kukamilisha miradi inayoendelea na kuanza miradi mipya katika kuboresha huduma ya maji katika jiji la dar es salaam.

Kuanza ujenzi wa miradi ya maji kutoka ziwa victoria kwenda maeneo mbalimbali ikiwa pamoja na mji wa mwadui na kishapu.

Miradi ya maji mikoa na wilaya mpya.

Muwezeshaji akiwa anatoa elimu kwa walioudhuria semina

 Miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya maji na umwagiliaji ni upungufu  wa wataalamu 
wa katika idra hiyo kwa kuwa uhitaji ni mkubwa kuzidi waliopo. Kwa kuwa wanahitajika wataalamu 10,287 na waliopo ni 2,290 kuna tofauti ya wataalamu 7,997 katika sekta hiyo.

Uwekezaji mdogo katika sekta ya maji na umwagiliaji  kwa kuwa Tanzania ina hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na hadi sasa eneo linalomwagiliwa ni hekta 461,324 sawa na asilimia 1.6 ya eneo lote linalichangia chakula cha nchi nzima kwa asilimia 24.

Kuweka vipaumbele vingi na hatimaye kushindwa kuvitimiza kwa asilimia kubwa hii ikia ni kuweka vitu vichache kama vipaumbele ili kuweza kuvitimiza kwa urahisi. Na siyo kuweka kila kitu ni kipaumbele mwisho miradi kuishia kati bila kumalizika kwa kisingizio cha bajeti kutotosha.

Kuhujumu kwa miundo mbinu ya maji na madeni makubwa kwa taasisi na idara za selikali.

Msafiri Shabani akichangia mada kwenye semina ya bajeti ya wizara ya maji na umwagiliaji

Kulingana na hayo yote MR Melikizedek ameishauri selikali  kupunguza vipaumbele na kuhainisha mambo machache kama vipaumbele ili kuweza kuyatimiza kwa urahisi.

Selikali kuweka bajeti halisi na kiwango stahiki ambacho inaweza kukipata na kupeleka kwenye wizara husika na  siyo inaweka bajeti kubwa na kushindwa kuitekeleza kwa asilimia kubwa kama ilivyoweka mwaka jana na ikaweza kutimiza kwa asilimia 19 tu.
Mkurugenzi mtendaji wa TGNP mtandao Lilian Liundi akichangia hoja

Wawezeshaji wakiorodhesha mapenekezo na matarajio ya wanaharakati

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.