Thursday, May 18, 2017

TRA YASAINI MKATABA NA BENKI YA KIBIASHARA YA TIB CORPORATE JUU YA UKUSANYAJI KODI

Benki ya bishara ya TIB corporate leo imeingia mkataba na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) lengo likiwa ni kusaidia walipa kodi kuweza kulipa kodi kwa urahisi zaid.

Benki hiyo ya kibiashara inayomilikiwa na serikali kwa 100% inayotoa huduma kwa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi. Na  kwa sasa benki hiyo ina  matawi 6 jijini Dar es salaam na matawi matatu yakiwa mikoa ya Mwanza , Arusha na Mbeya.

Kamishna mkuu wa TRA  Charles Kichere kulia akiwa na mkurugenzi wa benki ya TIB Corporate Frank Nyabudege wakitoa ufafanuzi juu ya mkataba walioingia TRA na TIB corporate
Akiongea na vyombo vya habari mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo alisema kuwa mfumo huu wa ulipaji kodi utasaidia kufanikisha malengo ya serikali katika kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi. 
Kamishana wa TRA akibadilishana nyaraka na mkurugenzi wa TIB corporate benki mapema jijini Dar es salaam

Waandishi wa habari wakiwa makini kusikiliza juu ya kusainiwa kwa mkataba wa TRA na TIB Benk

No comments: