Friday, June 16, 2017

CHADEMA WAIBUKA KIVINGINE LEO,KATIBU MKUU WAO AMVAA RAIS MAGUFULI MCHANA KWEUPE

DAKTARI  Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema dhamira ya Rais John Magufuli, kukabiliana na ufisadi haiwezi kufanikiwa iwapo ataendelea ubaguzi na uminyaji wa uhuru wa mawazo, anaandika Shafiyu Kyagulani.
Dk. Mashinji ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na wanahabari makao makuu ya chama hicho, Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa Chadema  inaunga mkono vita dhidi ya kutetea na kulinda rasilimali za nchi lakini inapinga vita hiyo inavyoendeshwa.“Ili serikali ifanikiwe katika vita hii ya kiuchumi, haina budi kuachana na kauli zake za ubaguzi kwa  watu walio na mtazamo tofauti na wake, Lazima Rais awaombe radhi watanzania kwa niaba ya chama cheke na awe tayari kuwajibisha kisheria.
“Viongozi wa serikali ya CCM ndiyo walioshiriki katika kufanikisha kuporwa kwa rasilimali za nchi, Rais Magufuli kama anataka kuchukua hatua basi asibague mtu au cheo cheke,” amesema Dk. Mashinji.
Ameshangazwa na nguvu inayotumiwa na Rais Magufuli kuvishambulia vyama vya upinzani na kutoa matamko yanayochochea uadui ilihali amekuwa akihubiri kila siku kwamba vita ya kiuchumi inahitaji umoja.
“Rais anaomba Taifa liwe pamoja katika vita ya kutetea rasilimali  zetu, hapo hapo anajenga na kuimarisha uadui kwa kila mwenye maoni tofauti na yake.
“Anasahau kuwa hata hayo anayofanya ni utekelezaji wa maoni na ilani ya vyama vya upinzani kwani ilani ya uchaguzi ya CCM ukurasa wa 26 mpaka 28 haizungumzii kabisa kuhusu kupiyia upya mikataba na sheria na sheria za madini,” amesema.
Amemtaka Rais Magufuli kuruhusu matangazo mubashara ya Bunge ili wananchi wenyewe wajionee mambo yanayoibuliwa na wawakilishi wao, huku aklitaka mikataba yote ilyokwisha sainiwa iwekwe wazi.
Katika hatua nyingine Dk. Mashinji amesema ipo haja ya Rais Magufuli kuufuta mchakato wa Katiba kwani Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi iliweka mapendekezo mazuri  juu ya namna ya kudhibiti rasilimali za Taifa.
“Ni vyema CCM na viongozi wake wajifunze kutokana na makosa kwa wanaendekea na kasumba ya kwuazomea wabunge wa upinzani pale wanapokosoa na kushauri wakati wa kupitisha sheria zinazokandamiza wananchi na kuacha mianya upotevu wa rasilimali za nchi,” amesema Dk. Mashinji.

No comments: