Chama cha Wananchi CUF baada ya mgogoro wa muda mrefu baina ya inayodaiwa kuwa CUF ya Maalim Seif na CUF ya Prof. Lipumba hatimaye muafaka umepatikana baada ya kupatikana Bodi ya Wadhamini inayotambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo June 21, 2017 DSM Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdallah Kambaya amesema.“Kutokana na mgogoro uliokuwepo ndani ya Chama au ambao upo ndani ya Chama ambao umepelekea baadhi ya Wanachama kwenda kufungua kesi Mahakamani na sisi kama viongozi kuwa watu ambao tunatuhumiwa kwa madai kadhaa.
“Mgogoro huu ulifikisha kuwa na vikao viwii vinavyojiita Baraka Kuu la Uongozi wa Chama Taifa. Kuna Baraza Kuu lililokuwa linaoongozwa na Katibu Mkuu na Baraza Kuu lililoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUP Prof. Ibrahim Haroun Lipumba.
“Mabaraza yote haya bila kujali uhalali upo kwenye Baraza lipi yaliteua Bodi ya Wadhamini na kuwasilisha RITA kwa ajili ya kuomba usajili kwa mujibu wa Katiba yetu. Tunachukua fursa hii kuwaeleza Watanzania, WanaCUF popote pale walipo na CUF Chama cha Wananchi kimepata Bodi mpya iliyosajiliwa na RITA siku nne tu baada ya yeye kuomba dua hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini mapema leo jijini Dar es salaam |
“Bodi hiyo inaongozwa na Peter Balebo Mwenyekiti lakini pia yupo Mkurugenzi wa Fedha Thomas Malima ambaye anakuwa kama Katibu wa Bodi. Kuna wajumbe wameainishwa, wametajwa hapa. Kwa hivyo, hivi sasa CUF Chama cha Wananchi kimekwishapata Bodi yake halali.” – Abdallah Kambaya.
No comments:
Post a Comment