Saturday, June 17, 2017

JUMUIYA YA KUHIFADHI QUR AN TANZANIA INATOA DOLA ZA KIMAREKANI ELFU 25 KWA WASHINDI


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amesema kuwa jumuiya hiyo imetenga kiasi cha dola za kimarekani elfu 25 kwa ajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanayotaraji kufanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Sheikh Kaporo ameeleza kuwa mashindano hayo ya sita kimataifa tangu waanze kuratibu yanataraji kuzishirikisha nchi 19 ambazo ni Kenya, Uganda, Mali, Nigeria, Algeria, South Africa, Bangladesh, Sudan, Kuwait, Libya, Djibouti, UAE, Russia Federation, USA, Yemen, UK, Dubai, Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar).
Displaying  Ambapo ameeleza kuwa matarajio yao yalikuwa ni ushiriki wa nchi 35 lakini baadhi yao ziliomba udhuru wa kutohudhuria kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wao.
Sheikh Kaporo amesema mgeni wa heshima katika mashindano hayo atakuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy akiambatana na mlezi wa Jumuiya hiyo Alhaj Ally Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheikh Kaporo ametoa wito kwa watanzania kuhudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo katika kumi la mwisho iliteremka Qur-an tukufu hivyo ni vyema wakahudhuria ili waweze kupata ujira kutoka kwa mola wao (Allah).

No comments: