BURUDANI

KALAPINA AANGUKA KWA MSANII TAMMY THE BARDEST


Msanii wa Muziki wa Hip Hop Nchini Tanzania KALAPINA Ametambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Demu mkali aliomshirikisha Rappa wa Kike kutoka Tanzania Tammy The Badest.

Akizungumza katika kipindi cha Kwetu Fleva kinachorushwa na Kituo cha Radio Magic Fm msanii huyo amesema ameamua kumshirikisha mwanadada huyo kwa kuwa ni ukweli kuwa Ni demu mkali anayemzimia kuliko wasichana wote wanaochana Tanzania.

"Tammy mi ndo msichana mkali sana kuliko wote wanaochana Tanzania,namaanisha mkali kwa kuchana,sura,umbo lake na kila kitu ni msichana mzuri sana,Wapo wengi wanachana ila wanakosa vitu flani anaweza akawa anachana ila Uzuri hana wengine Uzuri wanao ila Hawachanani sana ila Tammy ana vyote"ameeleza Kalapina wakati akijibu maswali katika kipindi hicho.

Kuhusu wimbo huo mpya ambao Kalapina ameuachia amesema kuwa Video yake itaanza kutengenezwa mwezi wa saba na mtengenezaji Msafiri shabani kutoka Kwetu studio na kwa sasa anakaribisha wasichana wanaojijua kuwa wao ni mademu wakali watume maombi ya kuonekana katika Video hiyo
Kabla ya Nyimbo hii Kalapina aliachia nyimbo ya kusifu Utendaji kazi wa Rais Magufuli,Japo haikufanya vizuri sana Nchini Tanzania.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.