Saturday, June 17, 2017

SHEIKH HEMED JALALA AMEWATAKA VIJANA WA TANZANIA KUTOJIHUSISHA NA UGAIDI

Vijana ni Tunu na nguzo ya Taifa, Taifa lolote duniani haliwezi kustawi pasipo mchango wa vijana kwani wao wanakuwa na fikra pevu na uwezo wa kuchanganua mambo kwa haraka zaidi kuliko wazee. Hayo yamesemwa usiku wa jana kwenye Semina iliyoandaliwa na Masjid Al Gadar uliopo Kigogo Dar es salaam. Semina hiyo ilijumuisha Vijana wanaoishi maeneo ya Kigogo na sehemu nyingine za karibu na Msikiti huo.

Sheikh Mkuu wa dhehebu la Khoja shia nchini Tanzania Hemed Jalala akisisitiza jambo kwenye Semina ya vijana iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam
Shariff Sagaff Ahmed akitoa elimu kwa Vijana walioudhulia Semina ya vijana iliiyofanyika jana jijini Dar es salaam
 Wawezeshaji wa semina hiyo ni Shariff Sagaff Ahmed kutoka Maande Islamic Centre akishirikiana na Mwalimu Kassim Hassan kutoka Shule ya sekondari ya Kibondo liyopo Kigoma na mwenyeji wao akiwa ni Sheikh Hemed Jalala. Kwenye Semina hiyo vijana walipewa elimu ya kujitambua na kufahamu nini majukumu yao kama vijana na kwa kiasi gani wanaweza kujiepusha na mambo ya anasa na kuwa na bidii kwenye kazi.

Pasipo kuangalia itikadi za kidini walialikwa vijana wa dini zote na walipewa elimu ya kumjua mungu kila mmoja kwa imani yake na kuepuka vishawishi na kazi zote za muovu Shetani. Pia sheikh Hamed Jalala alipenda kuwahusia vijana kutojihusisha na makundi mabaya kwani tatizo la ukosefu wa ajira isiwe kigezo cha wao kujihusisha na shughuli za ugaid pamoja na ujambazi ambao tunaona ukishamili kwa kwa kasi na watendaji wa hayo yote wakiwa ni vijana.


Na mwisho kabisa vijana hao walipata Futari kwa pamoja na Sheikh Mkuu wa dhehebu hilo la Shia Hemed Jalala pamoja viongozi wengine wa msikiti huo.

Mwl. Kassim Hassan kutoka shule ya Sekondari Kibondo akiwapa elimu vijana walioudhuria semina jana Kigogo jijini Dar es salaam

Vijana walioudhuria Semina ya vijana iliyofanyika Masjid Al Gadar Kigogo jijini Da res salaam

 

Vijana walioudhuria semina hiyo wakipata Futari pamoja na Viongozi wa msikiti huo jana jijini Dar es salaam



      
Baadhi ya vijana walioudhuria Semina wakipata Futari


No comments: