UZALENDO

BAKWATA WAMPA TUZO YA AMANI FREEMAN MBOWE

Jumuiya ya waislamu BAKWATA imemtunuku cheti cha amani (PEACE AWARD) Mbunge wa Hai na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni nchini na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mh. Freeman Mbowe baada ya kuuona mchango wake wa kupigania amani katika kipindi ambacho yupo katika uongozi.
Cheti hicho alichotunukiwa Mbowe kimekuwa ni ishara muhimu ya kuonesha thamani ya mchango wake kupitia nafasi zake za kisiasa na uwakilishi ikiwa kuwa hasa katika kudumisha umoja, upendo,  haki, amani, mshikamano, ushindani wa hoja na kadharika kwa ajili ya wananchi wa Hai na Tanzania kwa ujumla.
Amani ya taifa lolote ina pande mbili na iko kama shilingi hivyo Mh. Mbowe aaswa kuendelea mbele na kupigania amani ya taifa lake bila kujali Changamoto anazokutana nazo bali awe ngangari kuzikabili na kuzishinda “hiki cheti /tuzo ya amani (PEACE AWARD) iwe ni kichocheo cha kupigania haki, kwakuwa amani na haki ni pande mbili za shilingi moja.”
Watanzania nao wanatakiwa kikamilifu katika kupigania amani ya taifa lao kwa kutoa sapoti kwa serikali na viongozi wa maeneo yao kwani hii itachachua maendeleo ya kiuchumi kwa taifa zima na hivyo kustawisha maisha ya wananchi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.