Leo june 6 ikiwa ni siku ya Mototo wa Afrika Mtandao wa
jinsia nchini Tanzania TGNP ukishirikiana
na vituo vyake vya taarifa na maarifa umefanya semina iliyokutanisha wanafunzi
toka shule mbalimbali za jijini Dar es salaam. Kwenye semina hiyo kulikuwa wanafunzi toka shule ya sekondari Mabibo, Kivule
sekondari, shule ya msingi Mchangani na wenyeji shule ya sekondari Makumbusho. Lakini
pia walikuwepo viongozi mbalimbali kama Diwani viti maalum wa kata ya Makumbusho
Bi. Pilly Ochaya, Afisa ustawi wa jamii wa manispaa ya Kinondoni Bi. Editha Mbowe
na viongozi wa mitaa na kata ya Makumbusho.
Kwenye mkutano huo kumeibua changamoto mbalimbali zinazowakabiri
wanafunzi wa shule zote za sekondari na
za msingi. miongoni mwa changamoto kubwa inayoripotiwa ni upungufu wa matundu
ya vyoo kwa shule zote na hali hii inasababisha mazingira ya vyooni yasiwe
rafiki sana kwa wanfunzi hali inayosababisha magonjwa kama UTI n.k
Pia kutokuwa na uzio kwenye shule nyingi limekuwa ni tatizo
kubwa kwa kuwa wanafunzi wanazagaa
pasipo kuwa na sababu za msingi. Lakini pia inawafanya wanfunzi kushindwa
kuelewa kinachofundishwa darasani na (concentration )mawazo yanakuwa yapo kwa
vinavyofanyika nje ya shule.
Na tatizo lingine kwa shule ya Makumbusho ni mama Utamu
ameripotiwa kuwa kikwazo kwa shule hiyo kwani wanafunzi muda wa darasani
wanakuwa kwake wakinunu pombe kali(vileo). Wanafunzi wengi walisema kuwa baadhi
ya wanafunzi wanatoa tabia mbaya huko na kuja kuzileta hapo shuleni hivyo serikali
itumie nguvu kumtoa mama huyo asiendelee kuharibu wanafunzi.
Na ukiacha changamoto wanafunzi hao waliweza kuhainisha faida
mbalimbali walizozipata kupitia mtandao wa jinsia Tanzania TGNP na vituo vya
taarifa na maarifa. Miongoni mwa faida hizo ni kufunguliwa kwa choo
kilichojengwa katika shule ya Mchangani ambapo walimu walikizuia kisiweze
kutumika na badala yake kitumike cha zamani wakati kipya kimeshakamilika.
Na pia kitu kingine wanachojivunia ni kufahamu elimu ya
jinsia na haki za mtoto na hivyo kuwaelimisha watu wengine waliopo majumbani
wasiweze kuonewa na kufahamu wapi ni mahari sahihi pa kupatiwa msaada wa kisheria au kijinsia.
Wanafunzi wa shule ya ya sekondary ya Makumbusho wakiimba wimbo wa kuhamasisha Watoto kupewa haki zao za msingi kama elimu, kulindwa nk ikiwa leo ni siku ya Mtoto wa Afrika . |
Na mwisho kabisa Diwani viti maalum wa kata ya Makumbusho Bi.
Pilli Ochaya aliaidi kuzifanyia kazi changamoto zao na kikubwa alichikiomba ni
ushirikiano wao na yeye ili waweze kizitatua changamoto hizo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mchangani wakiimba wimbo kwenye Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika shule ya sekondari Makumbusho mapema leo jijini Dar es salaam. |
Wanafunzi wa shule ya sekondary Mabibo wakionyesha uwezo wao kwenye maigizo ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika. |
Wanafunzi wa shule ya sekondari makumbusho wakionyesha maigizo yao mbele ya Mgeni rasni Bi. Pilli Ochaya ambaye ni Diwani viti maalumu kata ya Makumbusho. |
Diwani viti maalum wa kata ya Makumbusho Bi. Pilly Ochaya akiongea na wanafunzi toka shule shule mbalimbali za jiji la Dar es salaam kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika. |
No comments:
Post a Comment