HABARI ZA KIJAMII

TGNP MTANDAO YATOA SEMINA KWA WAKAZI WA KIBO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP siku ya jana tarehe 30 mwezi juni umefanya semina fupi iliyofanyika maeneo ya Kimara kibo iliyokutanisha baadhi ya wakazi wa kata hiyo lengo likiwa ni kujadili ukatili wa kijinsia uliopo kwenye kata hiyo.
Bi. Agness Lukani akiongoza semina ya ukatili wa kijinsia kwa wakazi wa Kimara Kibo iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam
Akiongoza semina hiyo iliyodumu kwa takribani masaa mawili dada Agness Lukani aliweza kuibua changamoto mablimbali zinazowakabiri watoto wa kike pamoja wanawake kwa ujumla kutokana na ukatili wa kijinsia. Baadhi ya vijana waliweza kuainisha baadhi ya vitendo vya ukatili vinavyopatikana katika eneo hilo na miongoni mwake ni.

Baadhi ya vijana walioudhuria semina ya ukatili wa kijinsia wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa kwa njia ya Televisheni mapema jana Kimara Kibo jijini Dar es salaam
Vijana wengi kutelekeza familia zao hii inaonyesha ni sababu kubwa kwa wakazi wa eneo la kibo kwa kuwa unakuta kijana anampa mimba binti na hatimaye kukimbia hivyo kumuacha binti huyo kuishi na mimba hiyo kwa tabu mpaka anapojifungua na baadae akiona mtoto kamekua anakuja kudai mtoto wake.

Kupigwa kwa wanawake pia ni miongoni mwa aina nyingine ya ukatili ambayo inapatikana kwenye eneo hilo na mara nyingi unakuta ni wivu wa kimapenzi hii inasababisha mtoto wa kike kupigwa kwa maana nakuwa hana uwezo wa kupigana na mwanaume na mwisho binti anakaa kimya pasipo kutoa taarifa popote hali inyofanya kitendo hicho kuwa endelevu cha yeye kupigwa kila siku.

Tatizo la mimba za utotoni pia limeendelea kuwepo kwa wanafunzi na wasiwanafunzi kutokanana maeneo waliyopo kuwa ni mjini lakini pia shule kuwepo mbali, na uwepo vijiwe vya vijana wasio na maadili mazuri kuendelea kuwarubuni watoto hao kwa kigezo cha kutojua kuwa ni wanafunzi.

Tatizo lingine ni kupiga watoto kupita kiasi hii nayo imeelezwa kuwa ni miongoni mwa ukatili unaopatikana eneo hilo, pale ambapo unakuta mtoto anakosea mzazi anashindwa kumkanya au kutafuta njia mbadala ya kumrekebisha na kuona suruhu kwake ni kumpiga hali inayofanya kumuumiza mtoto na sio kumrekebisha kama anavyodhani.

Baadhi ya mabinti walipaza sauti zao na kusema kuwa wanaume wao huwa wanashindwa kuweka usawa na kuwanyanyasa wao kwa kigezo cha kuwa na hali ni ngumu na kuwaomba wenzi wao wavumilie, Lakini inapotokea wamepata pesa nyumbani hawaonekani, na ikitokea wamerudi nyumbani wakiwa wamelewa hali inayowanfanya kushindwa kuwaelewa wakati wanakuwa pamoja kwenye shida ila raha wanakula na wengine.

Baada ya kupata mafunzo yaliyotolewa kwa kupitia Televisheni ilifikia muda wa majadiliano, kujadili walichojifunza kupitia kipindi walichokiangalia kwenye Televisheni

Na mwisho wakazi hao wa kibo waliweza kuafikiana kuwa waadilifu kwa familia zao na kumchukulia mtoto wa mwenzako ni wakwako kuweza kumkanya endapo atakosea ili kuweza kupunguza mimba za utotoni na aina nyingine za ukatili wa kijinsia. Na kuendelea kupongeza jitihada zinazofanywa na mtandao wa jinsia TGNP kuwapa elimu ya kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia.

                         

                         

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.