MITINDO

‘Ubunifu chachu ya ukuaji sekta ya bima’

 Ubunifu unaojielekeza kuleta mabadiliko katika bima ndio msingi wa kukua kwa sekta hiyo kama anavyosema mtaalamu wa masuala ya bima. Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mwandamizi wa taasisi ya bima ya Resolution Insurance (RI) Mary Anne Mugo  katika mahojiano na mwandishi alisema kuwa  moja ya mikakati mikubwa ya kukuza sekta ya bima ni kupitia kuwa na  mkusanyiko anuai wa bidhaa na wakati huo huo kuwaelimisha wananchi umuhimu na usahihi wa kuwekeza katika kuwa na bima.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam  hivi karibuni  Mugo alibainisha kuwa  kutofahamu kwa wananachi umuhimu wa kukabiliana na majanga  ni moja ya sababu zinazosababisha sekta ya bima kutokua kwa kasi. Alisema kwamba bila kuwekeza  katika kuwaelimisha watu kuhusu huduma zinazotolewa, sekta hiyo haiwezi kutekeleza mchango wake katika kukua kwa uchumi na maendeleo ya nchi kwa jumla. Alidokeza umma sio tu kwamba ni lazima utaarifiwe kuhusu bima lakini pia uhamasishwe  kuziwekea bima mali zao pamoja na bima za maisha.

“Kuhamasisha kuhusu soko letu kumekuwa kunaendelea kwa kusambazia wamachama sio kwa Tanzania tu bali pia  nchini Kenya, Uganda Sudan Kusini  ambao ni wananachama wengine wa Jumuia ya Afrika Mashariki  ambako tunaendesha shughuli zetu,” alisema Mugo.

”Ufahamu kuhusu huduma na sekta pia ni muhimu katika kukua kwake  pamoja na uchumi wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla,” aliongeza na kubainisha kuwa sekta hiyo ya kifedha ni muhimu  katika Nyanja yoyote ile ya uchumi.
Mugo alitoa mapendekezo yake akisema, “Watu ni lazima wafahamishwe  mchango unaotolewa na mabenki, mashirika ya bima, mifuko ya pensheni, masoko ya mitaji, na hali kadhalika maduka ya fedha  kwa sekta ya fedha ni nyanja  muhimu katika kukua kwa uchumi na maendeleo.”

Resolution Insurance ilianzishwa mwaka 2008 kama kampuni ya udalali  lakini baadaye ilibadilishwa  na kuwa kampuni ya bima mwkaa 2012 na kwa kasi ilijipenyeza katika  soko la bima la ndani na ukanda, ambapo katika hatua za awali ilikuwa inatoa bima ya afya pekee. Hata hivyo  kwa mujibu wa Mugo, RI hivi sasa ina bidhaa nyingi kwa ujumla zinazohusiana na bima  zikiambatana na kuwakinga wateja  dhidi ya aina mbalimbali za majanga  ambayo vinginevyo yangesababisha  hasara  kama wasingekuwa wamejiwekea bima dhidi ya majanga hayo.

Alibainisha kuwa bima hizo zinahusu magari, afya, moto, ajali, mali, usafiri, (barabara, majini na angani) na nyingine. “Tumelenga mipango ya thamani ya sera ya bima ambayo inakubalika kwa mahitaji ya wateja wetu”, alisema Mugo na kuongeza kwamba kampuni hiyo ya bima hivi sasa inatoa  sera ya biashara ya jumla   isiyo katika madaraja ya tiba  ili kuongeza thamani ya uwiano na nafasi kuifanya kampuni kuwa kituo kimoja cha huduma zote kwa wateja wake.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, kwa ujumla bidhaa za bima isiyo ya tiba inajumuisha dhamana ya kuaminiwa, bima ya wacheza gofu, dhamana, uhalifu, bima ya vifaa vya kompyuta na umeme, makandarasi, majanga yote, amana za wafanyakazi, hasara inayosababishwa na moto, bima ya moto, bidhaa inayosafirishwa, kuharibika kwa mashine, bidhaa zinazosafirishwa kwa njia ya majini, fedha zinazosafirishwa, bima ya kituo cha  mafuta (petroli) na bima ya mitambo (bima zote).

Nyingine ni pamoja na bima ya kuta za vioo, amana za umma, fidia ya mfanyakazi, bima ya kaya, bima za magari ya biashara na magari binafsi. “Katika dhana ya kuhakikisha kuwa  wananchi wanaelewa  faida za bima tunaandaa mazungumzo kuhusu afya, mikutano na kupimwa afya bure, na kwa njia hii tunawashauri wateja wengi  kadri iwezekanavyo  kujiunga na mipango yetu ya bima”, alisema Mugo.

 Takribani  asilimia 0.7 ya upungufu katika pato la taifa  kunaufanya upenyezaji wa bima  kuwa mdogo ambapo wadau wa kisekta wanabainisha kuwa kukosekana kwa sera  ya taifa  kuwa ni miongoni mwa sababu zinazozuia kufikiwa kwa bima miongoni mwa wananchi. Hata hivyo Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ilikadiria kupenyeza kwa bima kukuwa kungeweza kufikia silimia 0.9 mwaka 2016.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo sekta ya bima Tanzania ina wachangiaji 30 katika soko. Sekta ya bima kwa upande wa kuenea kwa usajili imekua kwa kiwango cha asilimia 0.7 ya Pato Ghafi la Taifa (GDP) kwa mwaka 2015. Katika kipindi hicho bima ya maisha ilichangia  shilingi bilioni 0.3.
Mwaka 2014 kiwango cha jumla kilipanda kwa asilimia 17 hadi kufikia shilingi  bilioni 554.4 kutoka shilingi bilioni 474.1 kwa mwaka 2013. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kiwango cha bima  zilizokatwa nchini  kilipanda kwa asilimia 76 hadi 12,052/- mwaka 2014 kutoka 6,849/- mwka 2010.

Sekta hii inakadiriwa kukua kwa asilimia 18 kwa mwaka 2016 na kupenyeza kwa bima  kufikia asilimia 0.9 ya Pato Ghafi la Taifa (GDP). Kwa mujibu wa  shirika maarufu la bima duniani Swiss Re ni kwamba Afrika Kusini ambayo ni nchi iliyo na uchumi mkubwa barani Afrika  haishangazi kwamba  ilichangia asilimia 75 au dola za Marekani bilioni 51.6 ya bima zote barani humo  kwa mwaka 2013.

Mugo alibainisha kwamba sekta ya ndani ya bima inakua kwa kasi akisema kuwa  kuingia kwa  wadau wengi katika soko kutasababisha uwepo ushindani wa kupata nafasi ndani ya sekta hiyo yenye faida. “Ushindani ni mzuri katika biashara”, alisema Mugo na kuongeza, “ni kwa kuwa kila mara  inapokua ni wito wa kuzindua biashara ili iwe na ubunifu zaidi na uanzishwaji wa bidhaa kunakowapa  wateja huduma bora na nzuri.”


Ikiwa inakadiriwa kwamba mapato ya jumla yanayotokana na biashara ni zaidi ya  silingi bilioni 10.0, RI inajivunia kuwa na watoaji huduma  zaidi ya 300 kote nchini na waajiri zaiidi ya 80 inaonesha dhahiri kuwa ni moja ya mchangiaji  mkubwa katika sekta ya bima ndani ya nchi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.