Hatimaye Zari amefunguka mazito baada ya fununu zinazozidi kusambaa kwamba Ivan ali-fake kuugua kwake kwa siku 11 na kifo feki na mazishi feki yaliyofanyika huko Kayunga Uganda.Akihojiwa na TheUgandan kwa mara ya kwanza baada ya mazishi ya aliyekuwa mume wake Ivan,Alijibu maswali mengi aliyoulizwa likiwemo moja lenye utata zaidi kuhusu Mwili uliozikwa si wa Ivan bali ni wa Ali Sennyomo.
Katika kujibu hilo swali Zari alifunguka kuwa Ivan alikuwa na Identity mbili Yaani Kama Ivan Semwanga akiwa Uganda na Kama Ali Sennyomo akiwa South Africa na alibadilika kulingana na deals alikuwa anapiga.Na Huanza kutambulika kama Ali Sennyomo Kuanzia Airport yeyote SouthAfrica.Pia aliongezea hata alivyopita Entebe Airport juzijuzi alipita kama Ali Sennyomo na Pia madaktari waliokuwa wakimtibu SouthAfrica walikuwa wakimtibu kama Ali Sennyomo.
Pia Zari alisistiza kuwa alizikwa kule Kayunga ndiye Baba wa watoto wake.Pamoja na maelezo yoote fununu kuwa Kifo cha Ivan ni Feki zimeendelea kushika kasi.
No comments:
Post a Comment