Wednesday, July 5, 2017

BRITISH COUNCIL YATOA OFA BABU KUBWA MSIMU HUU WA SABA SABA

Leo ikiwa ni tarehe 5 ya mwezi julai taasisi inayotoa kozi za kiingereza na kuunganisha watu kupitia ubunifu pamoja na utamaduni toka nchini uingereza ya British Council. Leo imefanya mkutano na waandishi wa habari lengo likiwa ni kuwafahamisha nini wamekuja nacho kwa msimu huu wa saba saba.
Mkurugenzi Mkazi wa British Council Bi. Angela Hennelly akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mapema leo jijini dar es salaam na kushoto kwake ni meneja maendeleo wa British Council Bi. Amata Bosco 

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi mkazi wa British Council nchini Tanzania Bi. Angela Hennelly alisema kuwa wataendelea kushirikiana na taifa la Tanzania kwa wananchi wake kuhakikisha wanafahamu lugha hiyo ambayo imekuwa ni lugha ya kibiashara na kutumika maeneo mengi zaidi duniani.

Na kuendelea kusema kuwa “Tunaipenda serikali ya Tanzania, kwa kuwa britishi council ipo hapa kwa sasa ni takribani miaka 47 tunasaidiana katika kusimamia mitihani mbalimbali pamoja na kutoa kozi za kiingereza” alisema Angela Hennelly
Baadhi ya vijana walioudhuria zoezi hilo la kufanya mtihani bure kupitia banda la British Council lililopo kwenye hema la Jakaya Kikwete mapema leo Saba Saba jijini Dar es salaam 
Akiongezea mkurugenzi wa biashara na maendeleo Bi. Amata Bosco alisema kwa sasa British Council inatoa ofa kabambe kwa wateja wake ya kufanya mtihani bure kabisa kwa msimu huu wa Saba Saba ambao mtihani huo kwa kawaida unalipiwa shilingi elfu 48 hivyo ukiwahi ndani ya Saba Saba utafanya bure kabisa bila malipo yoyote.

“Mtihani huo unakuwa ni kipimo cha kufahamu mwanafunzi anauwezo gani wa kufahamu lugha hiyo kabla ya kujiunga na kozi ya kiingereza na baada ya hapo mwanafunzi anatakiwa kwenda makao makuu ya British Council yaliyopo mtaa wa Ohio/Samora evenue kwa ajili ya kuanza kozi itakayoanza tarehe 24 mwezi huu wa 7”. alisema Amata

Lakini pia jambo lingine zuri ni wanamshukuru Rais wa Jamuuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuri kwa kuongeza muda wa kuwepo mahali hapo mpaka july 13 hivyo wananyongeza ya siku 5 za kuwepo Saba Saba. Na kwa hiyo wanawaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kwani hawajachelewa kuwahi ofa hiyo ambayo ni maalum kwa ajili yao.
Wananchi mbalimbali waliotembelea banda la British Council kujipatia huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye banda hilo mapema leo jijini dar es salaam

No comments: