Monday, July 10, 2017

DIWANI WA VINGUNGUTI MH. KUMBILAMOTO ATIMIZA AHADI ZAKE KABLA YA MIAKA MITANO KUISHA

Diwani wa kata ya Vingunguti ambae pia ni Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Bw. Omary Kumbilamoto alifanya mkutano wa adhara na wananchi wake lengo likiwa ni kukamilisha ahadi zake zote alizoziahidi kipindi anaomba kura.
Diwani wa kata ya Vingunguti ambae pia ni Naibu Mstahiki Meya wa Ilala Mh. Omary Kumbilamoto akiongea na wananchi wa kata hiyo mapema jana jijini Dar es salaam.

Kwenye mkutano huo uliokutanisha viongozi mbalimbali wa kiserikali, wamichezo na wavyama tofauti tofauti vya siasa kwa kuweza kumtia moyo kiongozi huyo ili azidi kufanya kazi nzuri kwenye kata yake na  taifa kwa ujumla.

Akiongea na wananchi wa kata hiyo ya vingunguti Mh. Omary Kumbilamoto alisema kuwa amekuja kuhitimisha kwa kile alichokiahidi wakati wa kampeni zake, kwa kuwa aliahidi kuwapatia gari la wagonjwa(Amburance) na kweli gari alileta baada ya kugundua kuwa Zahanati yao inakabiriwa na tatizo hilo.
Mh. diwani wa kata ya Vingunguti katikati akiagalia burudani zinazoendelea kwenye mkutano aliouandaa kwa lengo la kuamlizia ahadi zake alizoahidi kwa wananchi wake na kulia kwake ni Rashidi Matumra na kushoto ni Naibu Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Mh. Mussa Kafana
Lakini pia aliahidi kuboresha Zahanati hiyo ya Vingunguti baada ya kugundua kuwa zahanati hiyo inahudumia wakazi wa Vingunguti na hata wengine kutoka maeneo ya Kisarawe, Mkuranga na maeneo mengine. Kwa kuweza kuipanua hodi ya wazazi kwani hapo mwanzo ilikuwa inazalisha mtu mmoja hadi wa wawili kwa mwezi na kwa sasa inapokea wagonjwa wanne hadi watano kwa siku wanaojifungua.
Naibu mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Mh. Mussa Kafana akikabidhi zawadi ya jezi kwa moja ya makocha wa timu za vingunguti.
Na aliweza kutoa mahitaji yote ya msingi kwenye Zahanati hiyo kama Vitanda kwenye hodi ya wakina Mama, lakini pia mashine ya kufulia na kuachana na kufua kwa mikono, mashine ya kufua umeme(Generator) kwa dharula kwani umeme ukikatika inalazimika wagonjwa kutibiwa na mishumaa, laikini pia Tv na Feni kwenye hodi zote.
Diwani wa viti maalum kata Upanga Mh. Rukia Mohamed akikabidhi zawadi ya jezi kwa mmoja wa viongozi wa timu zinazopatikana kata ya Vingunguti 
Diwani Kumbilamoto alipongeza jitihada za serikali za kutunza mazingira na kwa hili aliweza kuvirejesha upya Vyoo vilivyojengwa kwa msaada wa Benki ya dunia na kushindwa kutumika kwa kukosa maji, ambacho choo cha kwanza kipo eneo la Machinjioni na cha pili kipo eneo la Relini hivyo akishirikiana na wadau mbalimbali wameweza kuviwekea maji na kwa sasa vinatumika.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Vingunguti wakifurahia baada ya kukabidhiwa kadi za chama cha CUF

Na kufikia leo diwani ndipo anakuja kumalizia ahadi yake ya mwisho kwa kuwa aliahidi vitende kazi wa wanamichezo ikiwemo jezi na mipira kwa wachezaji wa timu za vingunguti.

Msanii wa Singeli anaefahamika kwa jina la Mc Sudi aka Babu wa Loliondo akitumbuiza kwenye mkutano ulioandaliwa na Diwani wa Vingunguti.

No comments: