HABARI MPYA

KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI MH. ELISANTE OLE GABRIEL AONGEA NA VIONGOZI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA E FM NA TV E

Leo ikiwa ni tarehe 27 mwezi wa 7 ni mwanzo wa ziara ya Katibu Mkuu wa wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na michezo Mh. Elisante Ole Gabriel akitembelea vyombo mbalimbali vya habari vya hapa jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo iliyoanza kwenye kituo cha Efm radio pamoja na TVE vilivyopo Kawe jijini Dar es salaam lengo la ziara hiyo ni kuangalia ufanisi pamoja na kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa vyombo hivyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh.Elisante ole Gabriel akiongea na wafanyakazi wa Efm na TvE mapema leo kwenye ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari vya jiji la Dar es salaam
Akiongea kwenye mkutano mdogo uliofanyika kwenye makao makuu ya Efm Mkurugenzi Mtendaji wa Efm Bw. Denis Busurwa alisema kuwa kwa sasa Efm inasikika kwenye mikoa sita ikiwa Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Pwani na Tanga.

Na lengo likiwa ni kufika mbali zaidi ya hiyo mikoa waliyopo na kwa sasa wamefanikiwa kuajiri vijana 110 na kati ya hao asilimia zaidi ya 99 ni Watanzania na kwa upande wa TVE kutokana imeanza hivi karibuni inaajumla ya wafanyakazi 20  lakini lengo ni kuajiri wengi zaidi ili kusaidia kutoa ajira kwa vijana Wakitanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Efm radio na TvE Bw. Denis Busurwa akiongea kwenye Tafrija fupi ya kumkaribisha katibu mkuu wa wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo iliyofanyika makao makuu ya Efm Kawe jijini Dar es slaam

Lakini pia mkurugenzi mtendaji wa Efm alimuomba Mh. Elisante mambo kadhaa ikiwa zinapotokea nafasi za vijana kwenda kujiendeleza nje ya nchi(scholarship) zinapotokea waweze kupatiwa na wao au kwa kuweza kupewa kipaumbele ili vijana wao wakajifunze vitu vingi zaidi kuhusu taaluma yao.

Na pia katika kuunga mkono serikali ya awamu ya tano na kauli mbiu yake ya serikali ya viwanda wao kama Efm na TvE kwa pamoja wanaomba kushirikiana serikali ili kuangalia wafanye nini ili  Agenda hii iweze kuwa kubwa zaidi na isimamiwe kikamilifu.
Baadhi ya wafanyakazi wa TvE na Efm wakimsikiliza katibu mkuu wa wizara ya habari Sanaa Utamaduni na Michezo kwenye ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vya jijini Dar es salaam na leo ikiwa ameanza Efm radio na TvE
 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Elisante ole Gabriel alisema mambo mbalimbali waliyoyaomba atayachukua na ataenda kuyafanyia kazi na alipenda kuwaomba uongozi wa TvE na Efm kujitahidi kufika na mkoa wa Dodoma kwa kuwa kwa sasa fursa nyingi zimehamia Dodoma ikiwemo serikali yenyewe.

Na alipongeza jitihada za uwekezaji mkubwa uliofanywa na Efm kwani kwa watu wengi udhania kwamba Efm ni kitu kidogo lakini kwa yeye amegundua kuwa ni taasisi kubwa iliyowapa ajira vijana wengi wa kitanzania kupitia vituo vyake vya Efm na TvE.

Lakini pia bw. Elisante Ole Gabliel aliuomba uongozi wa Efm kuwajali wafanya kazi wake ili waweze kupata matunda mazuri zaidi na kwa kuwa wao wanategemeana kwani bila wafanyakazi hakuna radio na bila radio hakutakuwa na haja ya wafanyakazi.

Na kitu kingine alikipenda kwa media hiyo ni kuwa na maadili mazuri na miiko ya kazi hali inayofanya ufanisi kuwa mkubwa mahali hapo na kuwa wanakubali kurekebishwa pale wanapokosea.

Na Mh. Elisante alipenda kutoa rai kwa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii kwani ndio msingi wa maisha yao na pia inasababisha Efm na TvE wigo wake kuongezeka na wao kupata sifa na maslahi mazuri kwani uzalishaji ukiwa mkubwa hata maslihi yao yatakuwa makubwa.
Katibu mkuu wa wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Elisante ole Gabriel akkiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Efm pamoja na TvE
Pia kiongozi huyo alipenda kuwasihi kuwa ni watu wa kujari muda kwani muda ndio kila kitu na wakiweza kulikabili swala hilo itapunguza majukumu yasiyo ya lazima ya kiongozi kuangali muda ambao wafanyakazi wanafika.


Na jambo la mwisho aliwasihi kuweka Uzarendo mbele kwani wao ni tegemeo kwa Taifa hivyo wao wakitetelesha Amani iliyopo nchini wataleta madhara makubwa kwa taifa na pia hata maafa yakitokea hata na wao hawata nusurika kwani na wao ni sehemu ya Tanzania.
Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Efm Radio mapema leo jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Efm Radio Francis Ciza akipeana mkono na katibu mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Elisante ole Gabliel ikiwa ni baada ya ziara yake aliyoifanya Efm na TvE mapema leo jijini Dar es slaamAbout vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.