BURUDANI

MR T - AMALIZA UTATA KUHUSU P FUNK NA MASTER J

Producer anayefanya vizuri  kwa sasa aliyetengeneza ngoma zinazofanya poa kwenye  game ya Bongo fleva kama Nisaidie kushare, Bongo bahati mbaya, Mazoea ya Billnas na nyingine nyingi anayefahamika kwa jina la Mr T touch amemaliza utata kuhusu swala la producers wa sasa na wakitambo..

Mr T alisema kwamba hata atokee producer mkali vip hawezi kubadili historia iliyowekwa na Maregendary wa muziki wa Bongo ambao ni master J na P Funk wataendelea kuwa Icon ya muziki bongo fleva.

Akiongea kwenye kipindi cha E-news kinachorushwa na East Africa Television leo asubuhi Mr T alisema watu hao wanapaswa kupewa heshima yao kwa kuwa ndio waanzilishi wa bongo fleva na sisi wengine tulipata mwanga kupitia wao ndio maana kila tunchokifanya inakuwa ni kama marudio tu.                        ENDELEA KUTEMBELEA HABARI 24 KWA HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.