SIASA

MRITHI WA MGHWIRA ACT WAZALENDO AANZA ZIARA YA MIKOA SABA KUKAGUA UHAI WA CHAMA

                                              
KAIMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo,ndugu Yeremia Kulwa Maganja,ataanza ziara rasmi ya mikoa saba ya Tanzania bara kwa ajili ya kukagua uhai wa chama na maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya chama ambao upo katika ngazi ya mitaa kwa sasa.
Katika ziara hiyo ya  Mwenyekiti Maganja itakayoanza Julai 17 Mwaka huu katika mkoa wa Mara pia atafuatana na katibu wa kamati ya kampeni na uchaguzi ndugu Mohamed Massaga Massaga, ambapo watakutana na kikao na kamati ya uongozi ya mkoa na majimbo yote ya mkoa Mikaoa mingine iotakayofikiwa katika ziara hiyo ni Simiyu (Julai 19),Shinyanga (Julai 20),Mwanza(Julai 21),Manyara (Julai 23),Arusha(Julai 24) na Kilimanjaro (Julai 25)
Baada ya ziara hiyo na itakayofuatiwa na tathmini ya kina Mwenyekiti Maganja atamalizia mikoa iliyosalia ya Tanzania bara kabla ya kuelekea mikoani kwa ajili ya kujitambulisha rasmi
Ziara hii ya Mwenyekiti Maganja itakuwa ni ya kwanza kwa kiongozi huyo ambaye alipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa Mama Anna Mghwira, aliyeondolewa katika nafasi hiyo na kamati ya uongozi ya chama baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mkuu wa  mkoa wa Kilimanjaro.

Imetolewa na Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT Wazalendo
14/07/2017

0655 549154

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.