Saturday, July 15, 2017

ORODHA YA MAJINA AJIRA MPYA ZA WALIMU MASOMO YA SAYANSI SHAHADA NA STASHAHADA AWAMU YA PILI 2017

Ajira Mpya za Walimu wa Sayansi ,Hisabati na Mafundi Sanifu

Walimu na mafundi sanifu watakao pokea posho ya kujikimu na baadae kutoripoti na kuanza kazi katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene leo katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma juu ya ajira mpya za walimu wa sayansi na hisabati awamu ya pili pamoja na mafundi sanifu wa maabara kwa mwaka 2016/2017.

Alisema walimu hao na mafundi sanifu wa maabara ambao wamepangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 17 - 31 julai 2017 na kwa wale watakao pokea posho ya kujikimu na baadae kutoripoti watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria .
� kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watumishi wanaopangiwa vituo vya kazi kupokea posho za kujikimu na kutokomea bila taarifa yoyote,hivyo basi niwasihi wale wote waliopangiwa waripoti mapema ndani ya tarehe hizo�alisisitiza
Waziri Simbachawene aliongeza kuwa watumishi hao wanatakiwa kufika kwenye vituo vyao vya kazi wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne na cha sita,cheti halisi cha kitaalam cha kuhitimu mafunzo katika ngazi husika na cheti cha kuzaliwa.

Vilevile alisisitiza kuwa walimu hao pamoja na wataalam wanatakiwa kuripoti katika ofisi za Wakurugenzi wa Halmasahauri husika na baadae kuripoti kwenye shule walizopangiwa na hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.
Aidha Mhe. Waziri aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo walimu na wataalam hawa wataripoti wawapokee kwa kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi na baadae kutoa taarifa mara baada ya tarehe ya mwisho ya kuripoti.

Walimu hao pamoja na mafundi sanifu wa maabara wametokana na tangazo la nafasi za kazi lilitolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia mwezi aprili 2017 , ambapo kwa awamu ya kwanza walipatikana jumla ya walimu 3,081 na kwa awamu hii Jumla ya walimu 381 na mafundi sanifu wa maabara 137 wamechaguliwa .
Majina ya walimu na mafundi sanifu walioajiriwa yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI.

No comments: