BURUDANI

RAMA D - AKEMEA WANAMUZIKI WANAOONYESHA VIUNGO VYAO KWA AJILI YA KUTAFUTA KIKI

Msanii wa Bongo Flava, Rama Dee amesema si vyema kwa wasanii kutumia kiki za kuanika maungo yao ya mwili hadharani ili kujitangaza kimuziki.


Rama Dee ambaye sasa ameachia wimbo mpya ‘Nibebe’, ameiambia Ladha 3600 ya E FM kuwa hadi kufikia hatua hiyo ni kwamba maudhui yamepungua katika muziki.
“So mpaka inafikia watu wanaamua kutumia njia za kulazimisha kama unaweza kuona dada zetu wanaonyesha maungo, wadogo zetu pia wanaonyesha maungo ilimradi vitu vikiki,” amesema Rama Dee na kuongeza.
“Sasa mimi nafikiri kitu ambacho ni cha msingi ni bora uonyeshe kazi kuliko maungo, hicho ni kitu cha msingi. Pia nafikiri na content nzuri zaidi, ubunifu na usiangalie mtu fulani kafanya nini, angalia wewe kitu gani unacho na kifikishe kwa watu halafu angalia watu wanachukuliaje, cha msingi kuwa wewe kwanza,” amesistiza Rama Dee.

About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.